OVC ni kifupisho cha Orphan & Vulnerable Children (watoto yatima na walio katika mazingira duni) ni mradi wenye lengo la kuwasaidia watoto wanaotoka katika familia masikini, yatima na wenye ulemavu kupata elimu bora kwa maisha yao ya baadae. KISEDET inawasaidia watoto kutoka shule ya msingi, sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa kuwalipia karo , sare za shule na mahitaji mengine ya shule.
Kwa watoto wanaoishi na wazee(babu/bibi) wasiojiweza, KISEDET hutoa chakula na huduma za kiafya (matibabu). Kwa watoto wote na vijana wanaosaidiwa na shirika, hupatiwa pia bima za afya kwa ajili ya matibabu.
Kupitia mradi huu, KISEDET pia husaidia shule za serikali kwa kuwapatia vitabu, madaftari, rimu, chaki, madawati (tunapokuwa na bajeti ya ziada) tunachangia katika ujenzi na ukarabati wa madarasa. Kwa miaka yote hii, KISEDET imeweza kutoa madawati 850 na kujenga madarasa 48 na ofisi za waalimu 15.