Shirika linawadau mbalimbali ambao pia ni chanzo cha fedha kwa shirika. Wadau hawa ni:
- Gruppo Tanzania Ets. Hawa ni sehemu ya shrike (kama dada) ambao wako katika mkoa wa Lombardia kaskazini mwa Italia. Wajumbe/wanachama wake wanatoka katika mikoa mbalimbali. Lilianzishwa kwa ajili ya kusaidia na kukusanya fedha za kusaidia shughuli mbalimbali za KISEDET Italia. Shirika hili ni chanzo kikuu cha fedha kwa KISEDET.
- Progetto Agata Smerrlda. Shirika hili linapatikana Florence, Tuscany katikati ya Italia. Walitusaidia kuchimba kisima cha maji katika makao ya watoto Chigongwe, kutoa gari aina ya coaster kwa ajili ya kubebea watoto, kusaidia na kendesha mradi wa OVC katika eneo la Itigi mkoani Singida na mradi wa vikundi vya kijasiriamali.
- Maria Centro Donna. Hawa ni rafiki zetu wa kike kutoka mkoa wa Lombardia kaskazini mwa Italia, wanaendelea kuisaidia KISEDET hasa katika shughuli ya ujenzi wa kituo cha makao Chigongwe, walijenga jingo la kwanza ambalo kwa sasa linatumika kama ofisi.
- Arcobaleno su Tanzania. Ni muunganiko wa waitaliano kutoka mikoa ya Gallipoli na Puglia kusini mwa Italia. Wanaisaidia KISEDET katika shughuli nyingi ikiwemo ujenzi wa kituo cha makao ya watoto Chigongwe, na pia wanasaidia uchimbaji wa bwawa la kufugia samaki.
- USAID/PACT na Railway Children Africa ni wadau wa KISEDET katika mradi wa Kizazi Kipya.
Shukurani za dhati kwa benki ya Barclays, Zanzibar Insurance Corporation na watu binafsi wanaojitoa kutusaidia kwa namna moja ama nyingine.