Help street children in Tanzania

Home>Habari>Uncategorized>Ugawaji Vyerehani Kwa Vijana Sita

Tarehe 11 March 2021, KISEDET ilikabidhi vyerehani kwa wasichana sita mbele ya Afisa wa serekali idara ya maendeleo ya jamii Dodoma (Afisa maendeleo jiji)

Wasichana hawa walimaliza mafunzo ya ushonaji nguo ambayo yalikuwa yamefadhiliwa na USAID/PACT pamoja na KISEDET.

Walianza mafunzo wakiwa kumi, lakini waliomaliza mafunzo  walikuwa sita tu. Watatu kati yao wanaishi na watoto bila waume zao (mzazi mmoja), wanaishi vijijini na/au maeneo mbalimbali ya Dododma pamoja na watoto wao na wazazi wao. Mafunzo hayo yatawasaidia katika maisha yao ya baadae ili wajitegemee na kuweza kasaidia/kuhudumia familia zao.

Mmojawapo ambaye ni Gaudencia, alisoma fani ya ushonaji kwa miaka mitatu katika chuo cha “Umoja wa mafundi” na kuweza kuhitimu. Shukurani za pekee kwa Gruppo Tanzania ETS ambao wamemsaidia kwa muda mrefu mpaka kuweza kumaliza mafunzo hayo na ambao huwasaidia watoto kusoma mpaka kufika elimu ya juu, (Vyuo na vyuo vikuu) kupitia ufadhili wao.

Kwa maelezo/taarifa zaidi wasiliana na Claudio +39 334 2136352 au tembela tovuti ya

www.grupootanzaniaets.it.