Salamu nyingi za pole zimetolewa kutoka Afrika na dunia nzima kufuatia kifo cha raisi John Pombe Joseph Magufuli. Alipokuwa madarakani, Magufuli alisimamia dhana za kiafrika, kupambana na rushwa na kujenga miundombinu.
Anayemfuatia ni Samia Saluhu Hassani, kutoka chama kimoja, ambaye alishawahi kufanya kazi za ushirikiano wa kimataifa. Hassan ni rahisi wa kwanza wa kike Tanzania. Kiukweli tunafurahi na matumaini, hii ni hatua mojawapo ya kuwawezesha zaidi wanawake katika taifa letu.
Hata hivyo katika makao ya Chigongwe, ujenzi unaendelea. Hapa wageni wetu watakuwa na sehemu tulivu ya kujifunza na maeneo elekezi ya kutembea nay a shughuli mbalimbali kama vile Yoga na hisia ambapo imethibitishwa kuwa inakubarika sana. Pia tumepanga kutumia sehemu sehemu jingo hilo kama nyumba ya wageni kwa ajili ya wanaojitolea na wageni wanaotutembelea, mradi huu utatusaidia kuendeleza upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi yetu. Ndani ya Chigongwe, tunachokilenga sana ni kuwa eneo la uzalishaji kupitia shughuli mbalimbali, sehemu ambayo watoto wetu watajifunza kwa vitendo katika shughuli za kilimo, upandaji miti, ufugaji wa wanyama na samaki na karakana ya uselemala. Kitu cha muhimu na cha kuzingatia ni kwamba watoto wanapewa mafunzo na kuelekezwa juu ya taaluma ambazo zitawafanya wawe huru na kujitegemea, na kuwafanya waweze kusaidia familia zao kama watapenda kufanya hivyo. Sisi kwa upande wetu, tunaamini katika ujasiliamali kuwa ni njia bora na hatua ya kwanza katika miradi yao. Kisedet imejidhatiti hivyo kutokana na matokeo ya taarifa mbalimbali kutoka kwa walengwa wetu waliofanikiwa: kama vile Saidi na Salumu ambao kwa sasa ni mafundi umeme, Jacob ambaye tunashukuru ana kazi ya uchomeleaji, na kwa sasa anaisaidia familia yake ambayo ni kubwa na Mrisho ambaye aliokolewa kutoka unyanyasaji wa kifamilia na sasa anaendelea na masomo katika tahasusi yake.