Vijana wawili walioruhusiwa kutoka Njiro sober house

Tarehe 7, Februari 2024 vijana wawili waliokuwa wakiishi na kufanya kazi mitaani waliondolewa katika Njiro Sober House, jijini Arusha. Vijana hao katika Sober House. Kutoka kushoto kwenda kulia: Hamisi, Rashidi, Kais, Mathayo na Stanley.

Kais na Stanley, walikuwa wameanza mchakato wa kuacha gundi na bangi. Waliruhusiwa baada ya tathmini iliyohusisha pande tatu: vijana wenyewe, msimamizi wa Sober House na Kisedet.

Tuliamua pamoja kwamba wakati ulikuwa umefika wa kuwaondoa vijana hao wawili na kuwaandikisha katika chuo cha ufundi ambacho kinatoa kozi za kutengeneza viatu na nguo. Chuo cha ufundi kinalenga kuwasaidia wanafunzi kupata ujuzi utakaowawezesha kujitetegemea.

Tarehe 9 Februari 2024 walengwa waliandikishwa kwenye shule ya ufundi Ambrosini, kinaendeshwa na Masista wa Santa Gemma. Tulikamilisha uhamisho haraka ili kupunguza uwezekano wa kurudi katika hali hiyo. Watafundishwa kozi tofauti kwa miezi sita, na baada ya tathmini wataamua ni fani gani watakayo endelea nayo.

Maisha ya Kais na Stanley ni kama yale ya watoto na vijana wengi wanaoishi na kufanya kazi mitaani na ni ya unyanyasaji na mateso.

Baada ya kuishi mitaani kwa miaka michache, Kais alipokelewa katika makao ya muda mrefu na ya muda mfupi ya KISEDET. Alirudishwa kwa familia yake, lakini baad ya muda, alirudi tena mitaani.
Baada ya kuishi mitaani kwa miaka kumi, Stanley alipitia hali ngumu sana ambayo ilibadilisha maisha yake. Baada ya kusingiziwa uizi , yeye na mvulana mwingine walipigwa sana na kumwagiwa petroli; kwa bahati nzuri, kiberiti hakikuwaka moto, na wakaweza kutoroka.

Walipofika KISEDET walipelekwa hospitali na kupewa matibabu. Walipotoka hospitalini, maafisa ustawi wa KISEDET waliwaambia wakaae katika makazi ya muda mfupi ya Shukurani.

Siku iliyofuata, mwenzake wa Stanley alirudi mitaani; tukampata baada ya miezi michache katika mortuary, akiwa ameuawa na watu wasiojulikana (tazama makala ya tarehe 02/16/2023).

Stanley aliweza kubaki na sisi na baada ya wiki tatu hivi, alienda kwenye sober house.

Je, Stanley na Kais watafanikiwa? Bado ni mapema mno kusema, lakini tunajua kwamba wanajitahidi sana kubadilika.

Kila la kheri wapendwa Kais na Stanley, muwe mfano kwa watoto na vijana ambao bado wanaishi na kufanya kazi mitaani na kwa vijana ambao bado wapo kwenye sober house.