Mara nyingi tunawahadisia kuhusu uunganishaji wa familia wenye mwisho wa furaha, lakini kwa bahati mbaya pia kuna wakati ambao familia bado ina matatizo mengi na baada ya muda, wazazi na watoto wanatengana tena katika hiyo familia.
Katika kesi kama hizi, KISEDET inabaki karibu na mtoto au kijana, ikiandamana naye kwa dhamira njema katika njia nzuri itakayomsaidia kuwa na familia yake. Mara nyingi, matatizo kwenye familia yanasababishwa na walezi au wazazi.
Mfano wa karibuni: familia ya watoto watatu, wavulana wawili na msichana mmoja, mama mmoja ila mtoto wa kwanza ana baba tofauti.
Muungano huo ulifanyika mwaka jana na mwanzoni ulikuwa wa utulivu sana: watoto walikwenda shule na yule mkubwa, baada ya kumaliza shule ya msingi, alianza masomo ya Pre Form I. Mama huyo alikuwa ameacha “kazi” yake ya mwanzo na kufanya kazi ya uadilifu zaidi: baadala ya kufanya ukahaba, alikuwa anapika chakula kwa mafundi ambao wanajenga nyumba mitaani kwa kutumia mtaji wa awali kutoka kwa KISEDET. Kwa njia hii, aliweza kulipia masomo ya mtoto wake mkubwa na kutunza familia nzima.
Walikuwa wakifuatiliwa kila wiki na maafisa ustawi wa jamii wa KISEDET na familia ikaanza kuungana na kuishi maisha ya kiheshima. Baada ya miezi michache, kulingana na itifaki, ziara za maafisa ustawi wa jamii, zikawa kila baada ya wiki mbili na kisha kila mwezi.
Siku moja, maafisa ustawi wa jamii wa KISEDET walifika nyumbani kwao bila taarifa na bila kupanga na waliwakuta watoto peke yao. Wakawauliza mama yao ameenda wapi, na watoto walijibu kuwa bado hajarudi kutoka kazini tangu jana. Wakazunguumza na majirani, na wakaambiwa kwamba mama huyo ameanza tena kujiuza, na kwamba watoto walikuwa wameacha shule.
Katika hali hiyo, KISEDET iliwasiliana mara moja na maafisa ustawi wa jamii wa serikali, ambao, kwa ushauri wa maafisa wetu, waliamua kuwaondoa tena watoto kutoka kwa mama yao ili waweze kurudi shule. Mkubwa hataki kusoma wala kuondoka nyumbani, huku wadogo zake wawili wenye umri wa miaka 11 na 9 wameandikishwa katika shule ya binafsi, takriban kilomita 300 kutoka Dodoma.
Tulichagua kusimulia hadithi hii kwa sababu mbili: kuonesha mojawapo ya hali halisi ya watoto tunaowasaidia na pia kuzungumzia jinsi ilivyo muhimu kudumisha usaidizi wa fedha. Watoto hao wamekuwa wakisaidiwa kwa miaka mingi na wafadhili wa Italia, kupitia mradi wa “elimu watoto”, lakini changamoto bado hazijaisha.
Kawaida, tunamjulisha mfadhili tunapoumuunganisha mtoto na familia yake. Wakati mwingine hutokea kwamba mfadhili huona kuunganishwa kwa familia ni kama kazi ya kumsaidia mtoto imeisha, hivyo hukatiza ufadhili, badala ya kumsaidia mtoto katika awamu mpya ya maisha yake pamoja na familia. Hali kama hiyo ilitokea miezi sita iliyopita kwa mfadhili wa mtoto wakike tunayemzungumzia hapo juu.
Kwa sasa ada ya mtoto huyu tunaipata kupitia wafadhili wote wanaotoa masaada kwa KISEDET bila kulenga mtoto fulani. Watu hawa, wanajua kwamba KISEDET inawasaidia watoto kulingana na mahitaji yao ya wakati huo.
Baada ya miezi michache, E. na kaka zake waliondolewa tena nyumbani na maafisa ustawi wa serikali na kukabidhiwa tena KISEDET (hadithi iliyosalia tayari imeelezwa hapo juu).
KISEDET inasisitiza kuwa mfuasi, ili awe hivyo, anaweza kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya miradi, si kwa ajili ya mtoto mmoja, bali kwa ajili ya kuendesha miradi ya kijamii ambayo mtoto anatokea.
Kulingana na sera ya KISEDET, na Sera ya ulinzi na usalama wa mtoto ya serikali, KISEDET inakataa kutumia picha za watoto kwa ajili ya kuchangisha fedha, bali picha za miradi ambayo watoto hawa wanahusika. Tunawashukuru wafadhili wote walioelewa na kushiriki chaguo letu, na tunawashukuru wale ambao watafanya hivyo katika siku zijazo.