Utumwa mpya

Wana miaka kati ya 12 na 17 na tayari watumwa wapya. Hawapelekwi Marekani lakini ni watumwa majumbani mwao, wakitumikishwa na watu wao.

Wasichana, wasiosoma au kwa sababu kadhaa waliacha shule na wametoka familia masikini ambao wamepelekwa kufanya kazi kwenye familia za kitajiri katika majiji makubwa ya Tanzania. Utumwa, bila mkataba, bila mshahara, anayefanya kazi kuanzia saa kumi na moja alfajili mpaka usiku katika mazingira magumu pamoja na unyanyasaji mkubwa: wa maneno, hisia,mwili na hata kingono na watu wa familia.

Kwa mwaka huu, KISEDET imepokea wasichana 12, walioopolewa kutoka mitaani na wasamalia waliowachukua majumbani mwao na kuwapeleka katika ofisi za serikali za ustawi wa jamii ambao kwa kutuamini waliwaleta KISEDET kwa ajili ya kufuatilia na kuwaunganisha na familia zao au shuleni au vyuo kujifunza biashara na kuwa na maisha yenye utu.

Mara kadhaa imetokea wamiliki wa nyumba (hasa wanawake) wamekuwa wakiwatoa njee na kuwafukuza usiku wa manane kwa sababu ya kuvunja kikombe, au mume wake kumnyanyasa msichana; na lawama haziendi kwa mume ila kwa msichana asiye na makosa. KISEDET inawatunza wasichana lakini inahakikisha serikali inafanya sehemu yake, kuhakikisha familia zinawaajiri, kutowatumikisha ili familia hizo zisifanye unyanyasaji badala yake wawaajiri watu wazima wafanye kazi za ndani.

www.kisedet.org