Mwezi mmoja uliopita, kikundi cha kwanza cha UCS wamerudi Italia. Walikaa Tanzania miezi 11. Hapa chini ni maoni yao.
SOFIA: “Kukaa mwaka mmoja Tanzania ilikuwa ajabu: nilipata fursa ya kuwajua watu wazuri, utamaduni wao na lugha yao (Kiswahili), na pia kujijua vizuri zaidi. KISEDET imekuwa ikifanya kazi na watu wenye uhitaji kwa miaka mingi, na ninashukuru sana kuwa sehemu ya kazi yao ambayo inaikumbuka jamii na kuheshimu utu na haki zao.
Huduma za kiraia ni fursa ya kipekee kwa ukuaji binafsi na wa kitaaluma. Nimeacha sehemu yangu Dodoma na Chigongwe, hakika nitarudi kwenye maeneo hayo na nitaendelea kuisaidia Gruppo Tanzania na Kisedet pia nikiwa Italia.”
GIORGIA: Mwezi Oktoba 2022 niliondoka Italy kwenda Tanzania kutekeleza Utumishi wa kiraia katika Shirika lisilo la Kiserikali la KISEDET na baada ya miezi 11 nilirudi Italia nikiwa na mzigo uliojaa kumbukumbu nzuri na uelewa.
Kutumia karibu mwaka mmoja katika nchi hii ya ajabu kulifungua macho yangu tofauti kabisa na vile nilivokuwa naona/kuelewa kwa kunipa mitazamo mpya na maoni. Kiuhalisia KISEDET bila shaka linahamasisha lakini pia linatoa changamoto: kufanya kazi na watoto na vijana wanaotoka kwenye mazingira magumu, shida na waliopitia changamoto mbalimbali lakini taaluma na shauku ya waendeshaji/wafanyakazi inahakikisha kuwa miradi mingi inatimizwa.
Huduma za kiraia kimataifa ni fursa ya kipekee na isiyoweza kujirudia kwa mtu yeyote ambaye anataka kushiriki katika ngazi ya kitaaluma na kibinafsi: pamoja na kufanya kazi katika KISEDET nimepata fursa ya kusafiri ndani ya nchi na kukuza mahusiano ambayo natumaini yatadumu milele. ASANTE SANA!
CHIARA: Mnamo Oktoba 18, 2022, niliondoka Italia bila matarajio mengi, sikutaka kuweka mipaka au shinikizo juu yangu mwenyewe kwa kile nitakachofanya. Na kwa hivyo, nilifika kwenye milango ya KISEDET kwa tahadhari.
Makaribisho yalikuwa mazuri sana, kila mtu alikuwa na shauku, mwenye hamu na utayari wa kunifanya nijisie huru, wanahisi kukaribishwa kama sisi ni wanachama wapya wa familia yao. Na hivyo ndivyo tulivyohisi, na tulielewa kwamba miezi hiyo 10 ingekuwa mizuri!
Zaidi ya tukio moja tulihisi tofauti za kitamaduni na njia tofauti ya maisha ya kila siku, lakini mara tu unapokumbatia roho ya “pole pole” na kuelewa kwamba haipo dhana ya “kila kitu mara moja”, utajikuta umezama katika ulimwengu wa machafuko na furaha.
KISEDET NGO na mwenzake wa Italia GR TZ ONLUS wana jukumu muhimu sana katika kusaidia watoto na vijana wa mitaani huko Dodoma (na kwingine). Hii ndiyo sababu nilijivunia na kuheshimiwa kuchaguliwa kuchangia kazi ambayo mashirika haya yamekuwa yakitekeleza kwa zaidi ya miaka ishirini. Kazi yetu haikuwa tu kazi ya ofisi, lakini tulipata fursa ya kuishi kwa ukaribu na wanufaika wa miradi.
Ni karibu mwezi mmoja sasa tangu turejee Italia. Naweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba wanachokiita “homesickness for Africa” ni hisia tu sio kweli, na hakuna siku inapita bila kufungua madirisha na kujikuta mbele ya mbuyu ambayo niliipenda kuiangalia kila asubuhi katika kijiji cha Chigongwe, Ilikuwa ni nyumbani kwetu, katika miezi hii ya Tanzania.
Asante Tanzania. Asante KISEDET. Tutaonana tena.
VERONICA: Kupata maneno ya kuelezea SCU ni ngumu. ukirudi nyumbani, hujui nini cha kusema, sio uzoefu tu, ni mwaka wa maisha, ambao unakubadilisha, mtazamo wako, maslahi yako na mawazo, hata bila kujua.
Ninaona fursa ya kuwa na wakati wa uzoefu ambao unanilazimisha kupigana na chuki na kujiweka katika viatu vya watu wengine: tabia ambayo lazima ifundishwe, hata kama wakati mwingine ni ya kuchosha.
Sio juu ya kuokoa mtu, ni juu ya kuelewa, kuchunguza, kuwa na uvumilivu, kusikiliza, kutoa muda kwa wavulana na wasichana, kutoa msaada na ushauri kwa wenzake, kupokea msaada na ushauri kutoka kwao, kukataa hukumu mbaya, kuzungumza, kujuana na kuishi pamoja kwa amani.
Ningechagua mradi huu mara elfu zaidi na ninawatakia kila la kheri SCU wengine.
Shughuli za KISEDET na juhudi za GR TZ za kukusanya fedha ni dhahiri na nitaendelea kuziunga mkono.
Mnamo Oktoba 4, SCU wapya walifika: Davide, Elisa, Simone na Agnese. Wataendelea kuwa nasi hadi tarehe 04 Septemba 2024.
Katika makala inayofuata tutakuambia juu yao.