Shirika lisilo la kiserikali la KISEDET limepokea cheti cha shukrani kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia kwa kutambua msaada mkubwa katika kuboresha huduma za jamii nchini Tanzania.
Siku ya Jumamosi tarehe 18 Machi, mkutano wa pili wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Italia yanayofanya kazi nchini Tanzania ulifanyika katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Rome.
Mbele ya Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo, na Dkt. Hassan Ali Hassan mkuu wa Kamisheni ya Uhamiaji Zanzibar, na Dk Anna P. Makakala wa Kamisheni Kuu ya Uhamiaji Tanzania, ya Balozi wa Tanzania nchini Italia Avv. Marco Conca kwa kuunganishwa kutoka Dar es Salam Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi – mkutano ulielezea kwa kina matatizo yote na maboresho yanayoweza kutokea katika mshirika ya Italia nchini Tanzania.
Mahmoud Thabit Kombo alithibitisha kuwepo kwa ushirikiano imara kati ya mashirika, wageni kutoka nchini Italia, vyuo vikuu na asasi za kiraia huku Marco Lombardi akisisitiza umuhimu mkubwa yaliyonayo mashirika yasiyo ya kiserikali ya Italia katika eneo la Tanzania, kuthibitisha ushiriki wa Shirika la Maendeleo la Italia (Aics) nchini Tanzania.
Lengo ni kuboresha na kuwezesha kazi kati ya mashirika na kuwa na lugha moja ya rejea inayoruhusu asasi kufanya kazi kwa sauti moja na kuwa na mahusiano na Serikali ya Tanzania.
Baadhi ya asasi zilizojipambanua kwa shughuli zao katika eneo la Tanzania zilitunukiwa na Balozi, kama vile Gruppo Tanzania Onlus ya KISEDET.
Giulia De Paolis alishiriki katika kikao kama makamu mwenyekiti wa Gruppo Tanzania Onlus kupokea cheti cha utambuzi na kueleza kutoridhishwa na ugumu tunaoupata kwa kuwapokea wataalam kama vile watumishi wa jamii kutoka Italia kutokana na kutoelewa na gharama na urasimu mkubwa unaosikitisha ambao hauoneshi utofauti wowote kati ya wafanyakazi wa ushirikiano wa kimataifa na wale wanaojihusisha na biashara.