Giovanna Moretti Mbeleje
MWANZILISHI NA AFISA UDHIBITI UBORA
QUALITY CONTROL OFFICER
Ni mwanzilishi wa shirika la Kigwe social economic Development ambalo lilianzishwa mwaka 1998 kijijini Kigwe kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu.
Anderson Andrea Ndonu
MKURUGENZI
Anashukuru sana Shirika la KISEDET kwa Ufadhili katika masomo yake mpaka ngazi ya Shahada katika kozi ya Utumishi na Rasilimali watu katika chuo kikuu cha Dodoma.
Fulgence Ado Nkane
AFISA UGANI na MANUNUZI na MHASIBU
Ana Stashahada ya uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anafanya kazi Kisedet tangu 2007. Anawasindikiza wageni wanaotutembelea kupitia mradi waatalii kupitia mradi wa "Tukutane Mbuyuni". Anafanya kazi ya uhasibu na pia anasimamia manunuzi ya vifaa katika miradi ya ujenzi na kuwasimamia mafundi.
Edwin Alphonce Shayo
AFISA RASILIMALI WATU & MHASIBU
Alizaliwa Arusha, ana Shahada ya menejimenti ya ushirika na uhasibu.
Anafanya kazi kisedet tangu 2018 kama Afisa Rasilimali watu na Mhasibu. Pia anasimamia miradi mbalimbali ya Shirika na anafanya kazi bega kwa bega na mashirika ya Italy Gruppo Tanzania Onlus na Agata Smeralda.
Hamisi Mazengo Ndoje
AFISA UIMARISHAJI UCHUMI WA KAYA NA FAMILIA
Kutokana na historia yake KISEDET iligharamia masomo yake yote mpaka ngazi ya shahada katika chuo kikuu huria cha Tanzania.
Mtahu Mtahu Muhibu
AFISA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO
Alisoma chuo kikuu cha Dar es salaam na kuhitimu mafunzo yake katika kiwango cha Shahada- Anafanya kazi katika idara ya familia na kufundisha elimu ya malezi ya watoto.
Isaac Abeli
Nsomi
MLEZI
Alihitimu masomo yake ya stashahada ya maendeleo ya jamii na baada ya hapo alijitolea KISEDET na baadae kuajiriwa na KISEDET kwa kazi ya mlezi.
Mwendwa Petro Mwihambi
MKUU WA MAKAO YA WATOTO YA MUDA MFUPI SHUKURANI
Alizaliwa Mvumi, katika Mkoa wa Dodoma. Watoto wanamwita Mama Mdogo, na anawasimamia akina mama ambao wanafanya kazi katika Makao ya Shukurani. Anawalea watoto na anapika chakula. Inapohitajika, anasaidia pia kazi ya ofisini.
Veronica Christopher Mdede
MAMA MKUBWA
Anawalea watoto katika Makao ya muda mfupi Shukurani, na pia anawapikia chakula watoto na wafanyakazi wa kisedet.
Alifanya kazi KISEDET hadi 2015, alipumzika kidogo kwa ajili ya shida ya familia, na kwanzia Novemba 2023 amerudi kazini.
Maimuna Iddi Kaluo
MAMA MDOGO
Anawalea watoto na kuwapikia. pia anawapikia wafanyakazi wa KISEDET.
Anafanyakazi KISEDET kwanzia 2015. Kabla ya hapa, alikuwa anafanya kazi katika nyumba za watu binafsi kama muhudumu.
Fredy Nyawange Mafuru
DEREVA
Alizaliwa Musoma, kanda ya ziwa. Alianza kufanya kazi KISEDET kwanzia 2021. Kabla ya kufanya kazi KISEDET, alikuwa dereva wa BOLT.
Joeli John Mihayo
DEREVA
Alizaliwa Moshi, katika Mkoa wa Kilimanjaro. Alianza kufanyakazi KISEDET mwaka huu 2023. Kabla ya hapa alikuwa dereva kwa watu binafsi.
Deusdedith Nkakya Rweikiza
MLEZI
Ni mlezi na Msimamizi wa mradi wa kitalu miti na ufugaji wa samaki KISEDET. Yupo na KISEDET tangu enzi ya Kisedet ipo Kigwe.
Yohana Petro Chimbwi
MTUNZA BUSTANI
Ni mtunza bustani za mbogamboga na matunda kwa ajili ya matumizi ya Shirika na ziada kwa ajili ya biashara.
Leah Katanga Mbutu
MSIMAMIZI WA MAKAO YA MUDA MREFU CHIGONGWE.
Pia anajulikana kwa jina la Shangazi, anawalea na kusimamia watoto na makao. Pia anafanyakazi ya bustani na kwenye mradi wa ufugaji kuku.
Sechelela Aine Mwiguti
MPISHI
Anawapikia watoto na wafanyakazi katika makao ya muda mrefu Chigongwe.
Skitu Japhety Mpangwa
MSAIDIZI KATIKA MRADI WA KILIMO.
Anafanya kazi KISEDET tangu mwaka 2020, anasimamia na kutunza vitalu miti na miradi mingine ya kilimo katika eneo la Chigongwe.
George Anderson
Machinda
MLINZI
Mlinzi wa usiku Chigongwe alipata mafunzo ya mgambo kwa muda wa miezi sita na baadae aliajiriwa na KISEDET.
Laurent Ezekia Mwaja
MLINZI
Ni mlinzi wa muda mrefu ndani ya KISEDET alianza kufanya kazi mwaka 2005 tangu enzi ya Kisedet ipo Kigwe.
Francis Mwaluko
Mwagulukuwawa
MLINZI
Ni mlinzi wa mchana kwenye nyumba ya mapumziko "Elena Fontana" ya KISEDET(Rest House) Alianza kufanya kazi mwaka 2022.