Mwaka 1996, mwanamke wa Kiitaliano Giovanna Moretti (Mbeleje) alisafiri kwenda Tanzania na marafiki zake wawili kwa ajili ya mapumziko. Walikaa wiki tatu katika parokia ya Kigwe kijiji kilichopo kilometa 30 kutoka Dodoma mji mkuu wa Tanzania. Kwa nini Dodoma? kwa nini Kigwe? Kwa sababu kule Italia walimfahamu padre Onesmo Wissi ambaye aliwaalika kutumia muda huo katika kijiji chake.
Mwaka 1997, Giovanna alirudi tena Tanzania na marafiki wengine, kukaa palepale kwa miezi mitatu. Wakati huo, kule Italia shirika lingine la Gruppo Tanzania Onlus lilianza kutafuta fedha kwa ajili ya watanzania kwa rasilimali chache.
Mwaka 1998, Giovanna aliamua kuishi Tanzania. Giovanna pamoja na viongozi wa kijamii Mzee Hamisi Nkopano na watu wengine walianzisha KISEDET.