Taarifa wa mradi Kizazi Kipya

Mradi ulianza mwaka 2017 mwezi wa tano na kufungwa mwaka 2020 mwezi wa tisa, ambapo mradi ulikuwa unashughulikia Watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Yafuatayo ni mafanikio ya mradi huo.

NoViashiria (Indicators)Mafanikio
1Utambuzi wa Watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mtaani1292 (799 me, 493ke)
2Kuwapatia Watoto makao ya muda mfupi231 (165 me, 48 ke)
3Huduma ya afya na huduma ya kwanza977 (658 me, 319 ke)
4Kuunganisha Watoto na familia zao191 (126 me, 65 ke)
5Kuwaunganisha vijana na mafunzo ya ufundi stadi273 (78 me, 195 ke)
6Kuwapatia vifaa vya kuanzia biashara kwa vijana baada ya kuhitimu masomo 132 (49 me, 83 ke)
7Kuwapatia wazazi mitaji ya biashara44 (7 me, 37 ke)
8Kutoa vifaa vya shule kwa Watoto waliounganishwa na familia zao Pamoja na ndugu zao wenye umri wa kwenda shule428 (320 me, 108 ke)
9Kutoa kadi za bima ya afya kwa vijana na watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani149 (52 me, 97 ke)

Baada ya mradi wa kizazi kipya kuisha shirika la Railways Children Africa (RCA), liliongeza muda wa miezi 10 (Julai 2021- May 2022) ambapo lengo la mradi huu ni kuzuia ongezeko la Watoto mtaani. Pia kufanya utambuzi wa Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani muda wote (Full time street).

Katika kuthibiti ongezeko la Watoto kuingia mtaani msisitizo upo katika kutoa mafunzo ya malezi salama (ACT TRAINING) kwa wazazi na walezi hasa katika maeneo ambayo yana uwezekano wa kutoka Watoto wengi.

Maeneo ya kufanyia kazi ni:

  • Kufanya utambuzi wa Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani
  • Kuwaunganisha na familia zao
  • Kutoa mafunzo ya malezi salama kwa wazazi na walezi
  • Kutoa vifaa vya shule
  • Kutoa huduma za afya
  • Kutoa mafunzo ya biashara na kutoa chakula kwa familia zenye uwezo duni Zaidi.

Changia