Shirikiana nasi

Saidia Kisedet: kiasi kidogo kinaweza kubadilisha maisha kabisa.

Tunategemea msaada wako, miradi yetu inaendeshwa kwa misaada/michango yako pamoja na ile ya wadau wetu wapendwa. Tunajitahidi kuwapatia watoto mwanzo wa maisha bora, nafasi ya kujifunza na kuwalinda dhidi ya hatari mbalimbali. Kila siku tunafanya kila kinachohitajika na watoto hata katika nyakati ngumu ili kubadirisha maisha yao. Lakini tunaweza kufanya yote haya pamoja nanyi.

Ungana nasi na uone jinsi gani inavyoleta faraja kwetu, kupata mrejesho kwa mmoja wapo wa mfadhili wetu:

“siku zote tunashangazwa na kuguswa tunaposoma na kuona namna mnavyopanga na kufanya shughuli zenu kwa kweli tunawapongeza.

Hakika tunafikirii kuwa tusingeweza kutumia vizuri kiasi kidogo cha fedha zetu, mbali na kuwapatia nyinyi KISEDET kwa ajili ya miradi yenu, katika miaka yote.

Tunapochangia fedha za misaada, tunafanya hivyo kwa nia njema na tunaamini zitatumika vizuri. Ni hakika kabisa tunajua mnachokifanya kwa ajili ya B. na kwa watoto wengine, na inaonekana kuwa mnaweza kufanya zaidi ya vile tunavyofikiri, kwa hiyo tunawatakia muendele na uzoefu wenu vizuri kuzidi kushirikiana na wadau wengine wenye mashirika yanayosaidia watu katika eneo mliopo.” Paola, Francesca na Maurizio

Shiriki, saidia KISEDET kubadilisha dunia, kwa mtoto mmoja.

Kwa mchango kidogo utakaotusaidia, utakuwa umesaidia ujenzi wa darasa zima, miradi midogo iliyopo shuleni au katika kituo cha watoto cha Shukurani cha KISEDET.

Nani yuko tayari kuwasiliana na kuikubali miradi yetu? Kama utahitaji kuwa mfadhili au kusaidia gharama za elimu kwa watoto au kwa kwa kazi yoyote inayofanywa na KISEDET, unaweza kuwasiliana nasi kupitia:

info@kisedet.org au info@gruppotanzaniaets.it

au unaweza kuchangia moja kwa moja Tanzania kwa njia ya simu au benki:

Lipa kwa simu, mitandao yote na benk kupitia namba 5590401 Kigwe Development

Watumiaji wa Vodacom M-Pesa
Piga *150*00#
1.Chagua lipa kwa M-Pesa
2.Ingiza namba ya malipo
3.Ingiza kiasi
4.Weka namba ya siri
5.Utapokea ujumbe kuthibitisha malipo
Watumiaji wa mitandao mingine.
Fungua menyu ya huduma za kifedha
1.Chagua kutuma fedha
2.Chagua mitandao mingine
3.Chagua m-pesa
4.Ingiza namba ya malipo
5.Ingiza kiasi na namba ya siri.
6.Utapokea ujumbe kuthibitisha malipo.
Au unaweza kuchangia moja kwa moja Tanzania kupitia Benki
KISEDET-KIGWE SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT AND TRAINING
BENKI :CRDB
TAWI LA CHAMWINO DODOMA
KWA WAGENI WALIO NJEE YA NCHI A/C 1952447960600 (kwa euro tu)
WALIO TANZANIA A/C 0150447960600
SWIFT CODE: CORUTZTZ 

Ufadhili