Nyonga pedeli pamoja nasi

Wasaidie watoto wa Tanzania kwenda shule!

Baada ya kuzungumza na baadhi ya watoto tunaowasaidia, tuligundua kwamba baadhi wao wanalazimika kutembea hadi kilomita 5 kwenda shule. Je, ungeweza kutembea kilomita 10 kila siku ili ufike shuleni?! Wakati wa kiangazi, ardhi huwa ina vumbi sana na wakati wa mvua, barabara huwa na matope mengi na unaweza kuteleza. Wanafika shuleni wamechoka na , wana kiu na njaa, hivyo hii inaathiri masomo yao na wanaweza pia kuacha shule.
Kwa sababu hii tuliamua kuanzisha kampeni ya ufadhili ya watu wengi ili kuweza kuwapa baadhi yao baiskeli hili kuraisisha safari wanayofanya.
Nchini Tanzania watoto husaidia wazazi na kazi za nyumbani, kwa hivyo, kuwa na baiskeli, itarahisisha majukumu ya familia na ya mtoto.
Kumiliki baiskeli ni muhimu sana, na mchango wowote utakuwa muhimu kuwapa fursa hii!
Dira ya KISEDET ni kusaidia maendeleo ya kijamii kupitia masomo na watoto ili watoke kutoka hali ya kimaskini.

UNAWEZAJE KUSAIDIA?
Tunataka kuchangisha Tshs. 1,900,000 kwa ununuzi wa baiskeli 10 aina za mountainbike (Tshs. 190,000 kila moja); Kwa kuwa barabara zina mashimo na matope, tunaamini kwamba aina hii ya baiskeli inafaa zaidi.
Kiasi chochote unachoweza kuchangia, kitathaminiwa sana na kingeleta mabadiliko makubwa kwa watoto hawa. Kama huwezi kuchangia, tunakuomba utusaidie kwa kushiriki kampeni hii na marafiki, familia au mtu yeyote unayefikiri anaweza kufurahi kutusaidia! Kadiri watu wanavyochangia, ndivyo tunavyoweza kununua baiskeli nyingi!
Asilimia 100 ya michango itaenda moja kwa moja kwa KISEDET kwa ununuzi wa baiskeli.

JIUNGE NASI!
Ili kuchangia na kupokea sasisho kuhusu mradi wa ufadhili wa watu wengi, jiunge nasi kwenye Instagram na Facebook na utembelee tovuti yetu.

“Elimu ndio silaha yenye nguvu zaidi inayoweza kubadilisha ulimwengu”
Nelson Mandela

https://buonacausa.org/cause/pedalando-insieme