Mtoto na ufadhili: kwanini tumeamua kusaidia jamii ya watoto na si mmoja mmoja

KISEDET walipendekeza kusaidia jamii kwa ujumla, na siyo mtoto mmoja mmoja. Yote hayo yalianza miaka kumi iliyopita wakati mradi wa watoto wa mitaani ulipoanza katika makao makuu ya Tanzania, Dodoma.

Mchakato wa kutekeleza, mikutano, makao, na uboreshaji wa ufanisi na muda (kila mtoto anayeishi na kufanya kazi mitaani, ana historia na mpango wake binafsi) kwa hiyo, kupitia uzoefu tumejifunza kwamba kuwalazimisha kubadilika kunaleta hatari kwao kuliko mazuri. Kwa maana hiyo basi, mfumo wa kuwa na mfadhili mmoja kwa mtoto ikawa ngumu, hivyo tukamua kuanzisha ufadhili kwa ujumla, itakayo saidia kugharamikia hatua mbalimbali za kuachana na maisha ya mitaani na baadae kuja kwenye vituo au makao yetu ambayo ni: Makao ya kutwa (Drop in), Shukurani (makao ya muda mfupi) na Chigongwe (makao ya muda mrefu).

Matokeo yake yamekuwa mazuri sana na wafadhili wetu wanafurahia kuendelea kufadhili mradi muhimu na wafanyakazi (maafisa ustawi) wa KISEDET wanafanya kazi nzuri na kutumia vizuri rasilimali fedha, na watoto wengi wameweza kuachana na mtaa na kuwa na nafasi ya kuanza upya. Pia tumeanza kuhamasisha ufadhili wa jumla hata kwenye maeneo ya elimu, badala ya kufadhili mwanafunzi mmoja, unaweza kufadhili Kijiji kizima au shule nzima. Hata hivyo mara nyngine ni muhimu kuwa na ufadhili wa mmoja mmoja kwa wale walio katika mazingira hatarishi zaidi.

Hii imetusaidia kuendelea kushirikiana na serikali za mitaa na kutufanya kuendelea kufanya kazi kulingana na sheria za Tanzania. Kama tunasaidia shule kujenga madarasa, maabara, madawati nk tunawasaida wanafunzi na walimu na mafanikio hayo yataonekana na kila mtu. Kama kuna mwanafunzi anayefanya vizuri kimasomo, tutamsaidia kuendelea na masomo yake na kupitia hayo tumepata matokeo mazuri. Tunaelewa kwa kufadhili mtoto mmoja inahamasisha zaidi na kutengeneza hisia zaidi hasa unapopokea taarifa na barua nzuri kila mwaka ya mtoto. Ni kweli kwamba malengo yetu ni kusaidia watoto/vijana wengi zaidi, kwa usaidizi wa jumla tumeweza kufanya hivyo. Wafadhili wetu wengi wamebadilika kufanya usaidizi wa jumla na tunafurahia uchaguzi wao na wanapoona michango yao imesaidia shule nzima inawafannya wajisikie fahari. Wanatambua kwamba ni washiriki mahili wenye ushirikiano na mradi. Shirikiana Nasi