Kupitia Shirika dada letu la Italia, Gruppo Tanzania Onlus, ambalo linatufadhili tangu 1998, Shirika la KISEDET limepokea awamu ya kuanza kutoka Waldesian Church, kwa ajili ya kuboresha Mradi wa kilimo na mifugo katika Makao ya Muda Mrefu, Chigongwe family.
Tangu tulipoanzisha Mradi huu wa Chigongwe family, Shirika limeanzisha miradi midogo midogo ya kilimo na mifugo ili watoto wapate chakula bora chenye virutumisho muhimu kwa afya bora. Ukubwa wa eneo ni 23 Ekta na asilimia 40 ni kwa ajili ya kilimo na mazao mbali mbali kama vile zabibu, miche ya miti na bustani ya mbogamboga.
Kupitia Mradi huu wa Waldesian Church, Shirika la KISEDET linataka kuboresha zaidi lishe kwa watoto na pia kuboresha ufugaji na kilimo bora.
Lengo kuu ni kupanua na kuboresha ufugaji wa kuku ambao tulianzisha mwaka 2020 kwa kujenga mabanda l ya kisasa na kuboresha mfumo wa umwagiliaji kwenye bustani na shamba.
Tutafuga kuku 400, kwa ajili ya mayai na nyama, ili tuweze kutumia ndani ya Makao na pia kuuza, ili tuweze kujitegemea, angalau kwa ajili ya chakula. Pia tunachotaka kufanya ni kuwapatia wananchi wa vijiji jirani, nyama na mayai fresh.
Tutawalisha kuku na vyakula vya asili (natural) na tutanunua vyakula hivi kutoka kwenye viwanda karibu yetu, kwa ajili ya kunyanyua pia uchumi wa jamii. Mbolea ya kuku tutatumia kwa ajili ya bustani na mashamba yetu.
Halafu, watoto na vijana wanaoishi katika makao haya, wataweza kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kwenye familia zao na jamii kwa ujumla.
Kazi ya ujenzi wa mabanda ya kuku, imeshaanza.
Tutatoa ya maendeleo ya mradi huu mara kwa mara.
Ukitaka kujua zaidi bonyeza hapa: Chigongwe