Mkutano mkuu wa wanachama wa Kisedet ulifanyika Alhamisi tarehe 27 Juni 2024.
Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Afya,
Mh. Dk. Godwin Mollel ambaye alitembelea makazi ya muda mrefu ya ‘Familia ya Chogongwe’, ambayo hupokea watoto na vijana kutoka mitaani na/au wale wanaotoka katika familia za kimaskini au wahanga wa ukatili wa nyumbani.
Pia aliweza kutembelea miradi mengine kama banda la kuku, mabwawa ya kufugia samaki, guesthouse kwa wageni, na kuzungumza vyema kuhusu miradi ya shirika.
Siku hiyo iliruhusu familia nzima ya Kisedet kukaa pamoja, wafanyakazi na wasimamizi, na pia wageni na UCS, na waliongelea na kujadili malengo ya kila siku ambayo shirika linajihusisha.
Haya yote yanaonyesha uthabiti wa shirika ambao wanapambana kila siku na umaskini na ukatili wa watoto.
Tunamshukuru Dr.Mollel na kila mtu anayeunga mkono na kufanya kazi pamoja na Kisedet!