Miaka 100 ya kuzaliwa: maadhimisho yataisha 2023

26th April 2022 imeandaliwa na Redazione Nigrizia.

Tanzania inaadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Julius Nyerere.

“Mwalimu Julius Nyerere (13th April 1922- 14th October 1999) anatambuliwa na watanzania wote kama baba wa taifa, ambaye waliadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake April 13. “ nawaalika watanzania wote kwa pamoja kusherekea siku hii iliyoandaliwa na waziri wa malia sili na utalii, Pindi chana”, alisema raisi Samia Suluhu Hassan wakati Raisi anaelezea maono na falsafa za Nyerere kama mwazalishi wa Tanzania ya leo. “Nyerere, raisi wa kwanza wa Tanganyika sasa Tanzania, ni mwafrika mzalendo aliyetoa Maisha yake kujenga taifa hili na kutengeneza umoja na utulivu katika nchi” aliongeza Samia wakati wa hutuba yake katika tukio mhimu la kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hili katika shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo wilaya ya Kibaha, mkoa wa Pwani.

Samia alisema falsafa hii ilitokana na mawazo ya “ujamaa”na inatekelezwa kwa maendeleo endelevu ya nchi hii. Maraisi waliomfuatia Nyerere – Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli na Samia mwenyewe wamejaribu kuendelea kufuata maono ya “Mwalimu” wakati wa uongozi wao.

Samia pia alisema mafanikio ya Nyerere yalibainishwa kwa maadui watatu kulingana na yeye kuwapinga kipindi cha uraisi wake- maadui hao ni maradhi, ujinga na umasikini. Kujenga shule, kufungua hospital na zahanati nchi nzima, kuwekeza kwenye sekta ya kilimo na miundombinu mengine yamekuwa ya muhimu kwa serikali zilizofuata baada ya Nyerere.

Pia alikuwa (kutokana na Samia)  akiheshimiwa na umoja wa Afrika, ambaye alitamani bara zima kuungana katika roho moja ya uzalendo na kuhamasisha umoja na amani kwa maendeleo ya Afrika.

Nyerere baadae aliacha majukumu yake kama mwalimu na kuungana kupigania uhuru wa Tanganyika uliopatikana 9 December 1961, na kuwa waziri mkuu wa na moja kwa moja alianza kulijenga taifa katika usawa na haki. “ urithi aliotuachia Mwalimu ni kazi ya kutengeneza usawa katika jamii ukiachana na tofauti za makabira, lugha, rangi na Imani za kidini.

Nyerere alikifanya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa na kwa sasa kinatambulika kama lugha rasmi katika umoja wa Afrika, umoja wa Afrika mashariki (EAC), Umoja wa maendeleo kusini mwa Afrika (SADEC). UNESCO imepanga kuanzia July 7 kuwa ni tarehe ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili.

Hii ni faida mojawapo ya Nyerere katika uongozi wake. Pia alitufundisha (licha ya wanasiasa wengi kujifanya kuwa wazuri) mnahitaji kutiwa moyo na kuwaambia sio sawa na hiki ni kitu muhimu unapotaka mabadiliko. Wazo la uhuru, umoja na maendeleo ambao ulikuwa msingi wa uhuru wa Tanganyika na baadae kuzaliwa Tanzania ndicho kinacho endesha nchi hii. Zaidi ya hayo na hekima, 2017 wajumbe 10 wa kanisa katoliki walimuomba Papa Francesco kubariki hekima hizo.

Kuhusu Sisi