Mauaji ya watoto wa mitaani

Hapa tuko tena, tukisimulia mauaji ya kikatili ya watoto wawili wa mitaani. Mara ya mwisho tulikuwa tumeanza kwa kutumia sentensi ile ile: “hapa tuko tena…”
Tunapaswa kuandika sentensi hii kwa muda gani? Ni lini “watu wasiojulikana” au umati uliokasirika utaacha kuua watoto wa mitaani?
Toma mwenye umri wa miaka 18, aliuawa jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita. Mwarabu mwenye umri wa miaka 17, aliuawa jijini Dodoma Desemba 6, ambaye mwili wake ulikaa kwa takribani miezi miwili katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya serikali, hadi baadhi ya marafiki zake walipoenda kuangalia kama mwili huo upo kwa sababu hawakumuona tangu alipopotea.


Mara ya mwisho kumuona Mwarabu ilkuwa mwaka jana, tulipomsihi abaki kwenye makao ya KISEDET, lakini jibu lake lilikuwa: “Siwezi kukaa hapa tena, maisha yangu ni ya mitaani sasa”. Tuliagana kwa kumwambia kwamba angeishia kama Jimmy na wavulana wengine wote waliouawa mtaani, lakini hata hili halikumshitua na hivi ndivyo ilivyoisha, kwa kusikitisha.
Tulikuwa tumemsihi abaki kwa sababu yeye na Stanley walikuwa tayari wamepigwa kikatili, na yeye, tayari alimwagiwa petroli, aliweza kutoroka tu kwa sababu watesaji hawakuweza kuwasha kibiriti kwa wakati. Ilikuwa jumapili mwezi Aprili tulipoambiwa, na tulipofika pale tuliwaona watu wawili waliojeruhiwa, tulibaki tumeshituka kwa alama za majeraha kwenye miili na nyuso zao.
Kitendo hicho cha kikatili kwa kuiba baadhi ya vyuma chakavu na vipuli vya magari. Tuliamua kukemea na kwenda kutuo kidogo cha polisi kilicho karibu na makao kwa sababu hatukuweza kwenda makao makuu tungepoteza muda kutokana na hali zao kuwa mbaya ingawaje kweli waliiba.


Tulipofika “tulikaribishwa” na polisi watatu, mmoja akiwa amevaa sare na wawili kawaida. Tukiwa bado tumesimama, tulianza kuwaeleza kilichotokea, lakini hawakuonekana kuwa wakarimu kwani mara moja walituelekeza twende kituo kikuu cha polisi. Tulijaribu kuwashawishi watusaidie (kwa Tanzania, tukio kama hili ukienda hospitali bila ripoti ya polisi huwezi kupata huduma), lakini hawakuonekana tayari kutusaidia. Kwa hiyo, mimi na mwenzangu tukaanza kuzungumza na punde wakaturuhusu kuingia.


Wakati huo huo, njee barafu ilivunjwa, pamoja na polisi wengine tulianza kujadili inawezekanaje watu waendelee kuua anayeiba au kutuhumiwa bila hata kujua kama wanafanya uhalifu. Mara baada ya kupata ripoti ya polisi, tuliwafikisha wale vijana hospitali binafsi, ambako tunamakubaliano ya kuwapata huduma za kiafya na baadae walikaa kwenye makao hadi walipopona.
Tuliwaita ndugu wa vijana hao, lakini ni mama yake Stanley pekee aliyejitokeza (familia ya Mwarabu inaishi Iringa), ambaye hakuwa na machozi tena ya kulia, alimwambia mwanae kuwa haya yalikuwa machozi yake ya mwisho kwani amekata tamaa na wakati mwingine atalia juu ya maiti yake. Majibu ya mama yake yaliamsha hisia za Stanley ambaye alionesha yuko tayari kwenda sober jijini Arusha. Kwa bahati mbaya, haikuwa hivyo kwa Mwarabu, ambaye aliondoka kwenye makao siku iliyofuata na hatukuonana naye tena mpaka mwisho alipoonekana katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Dodoma.


Tumechoka kulia dhidi ya watoto wetu, tumechoshwa kuhisi hatuna nguvu mbele ya vurugu kama hizi, tumedhamiria zaidi kuliko hapo awali kuendelea kuwapigania, kwa watoto wa mitaani, mpaka haki itendeke, mpaka wengine hawatauawa na mpaka wengine waache maisha ya mitaani, kama ilivyotokea tayari katika matukio mengi.


Roho zenu zipumzike kwa amani: Mauridi, Daudi, Danieli, Chuga, Boazi, Gidion, Antony, Peter, Aloyce, Agostino, Frankie, Johny, Ima, Jimmy, Toma, Mwarabu , Igidi.

Changia