Ally Mussa ana umri wa miaka 24, anaishi mtaa wa Chadulu, kata ya Tambukareli, Jijini Dodoma.
Kijana huyo alikaa kwenye Makao ya watoto Shukurani kuanzia mwaka 2011 hadi 2018 Alipokuwa akiishi katika Makao hayo alijiunga na shule ya msingi Chamwino kuanzia mwaka 2011 hadi 2015. Baada ya hapo alijiunga na Shule ya Ufundi pamoja na Sekondari St. Gabriel kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 lakini alipokuwa akisoma, aliacha shule na alianza maisha yake mwenyewe wakati huo huo alikuwa Dereva wa Pikipiki na Bajaji, mwaka 2020 alipata ajali wakati akiendesha Pikipiki na mwenzake aliyekuwa nayo na hali hiyo ilimfanya kuvunjika mguu na kupoteza mguu.
Tangu wakati huo KISEDET ilipopata habari hizo kutoka kwa wasamaria wema lilianza kumfuatilia na kuona jinsi tunavyoweza kumsaidia. Kisha hatua iliyochukuliwa kwamba Idara ya OVC ilifanya tathmini kwa Hospitali inayohusiana na matibabu yake. Hivyo, KISEDET ilitambua Hospitali ya Ikonda iliyopo Wilaya ya Makete mkoani Njombe na kijana huyo alisindikiza na kufanikiwa kuunganishwa na matibabu ya afya hasa kutengenezewa mguu wa bandia.
Mchakato unaendelea na ameanza mazoezi rahisi ya kutembea. Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini basi KISEDET itaona uwezekano wa kumsaidia vifaa anzia vya kuanzisha biashara ndogo ndogo.