Lugha ya Kiswahi itadumu?
Nilipofika kwa mara ya kwanza Tanzania, wanakijiji wengi na wakazi walikuwa hawawezi kuzungumza lugha ya taifa Kiswahili ila kigogo tu ambayo inazungumzwa katika mkoa wa Dodoma. Miaka 25 imepita sasa na mambo yamebadilika, watanzania wengi wanazungumza kiingereza au wanachanganya na Kiswahili. Swali ni kwanini? Inaonekana kama ni suala la kujidai.
Hapa watoto wanasoma shule ya msingi kwa miaka saba na wanafundishwa kwa Kiswahili. Kwa wale wanaosoma (kwa Tanzania miaka saba ya awali ni lazima) na watatumia miaka sita mengine kwa sekondari. Sifa ya mfumo huu ni kwamba walimu wanafundisha kwa kiingereza kuanzia sekondari hadi chuo kikuu. Labda utawaza “hii ina shangaza! Italy wataweza kufanya hivi”. Unaweza ukaona matokeo yake wanafunzi wengi wanashindwa kuendelea na masomo kwa kuwaza kushindwa kuzungumza kiingereza.
Mara kadhaa nimekutana na watoto ambao wananisalimia “Goodmorning teacher” wakati inakuwa jioni, inaonesha Dhahiri kuwa na ufundishaji mbovu wa kingereza shule ya msingi. Kiujumla ni kwamba hali ya Elimu Tanzania iko chini kidunia na sababu moja wapo nafikili ni kutumia lugha ya kiingereza badala ya Kiswahili, ukitoa upungufu wa vitabu, madawati, madarasa nk. Hata hivyo hakuna kilichofanyika mpaka sasa, lakini naamini serikali inalitambua hili.
Mbaya zaidi wazazi wanawapeleka watoto wao shule za binafsi na wanazungumza nao kiingereza hata wanapokuwa nyumbani. Wanajisikia fahari kuwa na watoto ambao hawazungumzi lugha yao ya taifa, bali lugha za kimataifa.
Ili kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili, turudi nyuma Julai 1954 wakati raisi wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere alichagua Kiswahili kuwa lugha ya chama, silaha kamili dhidi ya wakoloni. Baada ya uhuru 1961 shule, taasisi za serikali na mahakama ilikuwa ni lazima kutumia Kiswahili. Kampeni hii haikufanikwa kwa muda lakini kwa miaka iliyofuata mambo yalibadilika na sasa kiswahihili lugha rasmi ya kwanza kwa Tanzania, pia nchi chache za afrika zinazungumza lugha yao: swali ni kwamba, zitadumu?
Inasikitisha na kushangaza kutaka kusifia tamaduni za kimagharibi japo ndo uhalisia. Kuna migongano mingi katika nchi na mojawapo ya hiyo ni lugha, kwa upande mwingine idadi kubwa ya watanzania wa tabia ya ubaguzi wakidhani watu weupe ni wakoloni. Upande mwingine wako tayari kuuza historia na utu ili kuonekana kimataifa. Inawezekana hii tabia ni ya kidhaifu ambayo iliasisiwa kipindi cha biashara za watumwa kipindi cha ukoloni.
Kwa bahati mbaya miaka 500 ya utumwa haiwezi kusahaulika lakini hii haiwezi kuwa chanzo cha kuondoa uhuru wetu kwa sababu kuwajibikia historia. Hapa nashauri kusoma vitabu vifuatavyo: “Lettera alla tribù bianca” cha Alex Zanotelli.
Leo Italy lockdown imekuwa mbadala wa neno “chiusura, pub badala ya “birreria” nk sawa na Tanzania maneno ya kiingereza yanatumika kama mbadala wa kiswahili kwa mfano TV (runinga), glass badala ya bilauri, tren badala ya gari moshi nk. Kama hakutakuwa na mtu wa kuzuia mchakato huu baada ya miongo kadhaa kutakuwa na hali ya kukataa lugha yako na kupendelea za wengine.
Mbeleje