Dhana ya uraia ni bila shaka mada ya mjadala inaowahusu watu wengi. Umuhimu wa kutambuliwa na taifa ni haki ya kila mmoja. Kutambuliwa na taifa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya watu, lakini ni gumu kwa wengine. Mwanadamu, kama kiumbe wa kijamii, hupata maana katika kujiskia kwamba anatambuliwa katika kundi au jamii, ambapo anajihisi kuwa na starehe kutokana na desturi, mila, lugha, na tradisheni. Hisia hii ya jumuia na mali hairidhishwi tu na hisia ya mtu binafsi, na kujiskia kama mali na jamii ila ni jinsi ambayo watu na serikali inamtambua katika kundi/jamii na utambuzi wa uraia.
Duniani, kuwa na uraia fulani badala ya nyingine huwakilisha hadhi. Hebu tufikirie fursa zote zinazotolewa kwetu kwa kuzingatia utaifa wetu, kuanzia safari rahisi kwenda nchi za nje, fursa za ajira, uwezo wa kupiga kura na kuweza kuchangia kama sauti tendaji katika mijadala ya maamuzi yanayohusu maisha yetu.
Njia ambayo tunapata uraia, ni mada ya mjadala katika nchi nyingi duniani: Je, ni haki kupata uraia ya wazazi wako au kupewa ile ya nchi ulpozaliwa? Nini kinachotuunganisha na nchi? Nini kinatufanya tuwe wanaanchi? Haya ni maswali tata ambayo wataalamu kutoka dunia nzima wanajitahidi kujibu. Katika muktadha huu wa maswali makubwa ya kiitikadi, tunazungumzia pia hadithi za kweli, hadithi za maisha halisi ambazo ni muhimu na za kipekee kama zile zinazoakisi mifumo tata. Kuangalia mifano halisi ya maisha halisi ni lengo la makala hii. Alice na Valeria, watoto wa mwanzilishi na mwasisi wa KISEDET, walizaliwa na kulia Tanzania, wazazi wao ni waitaliano, wameishi maisha yao yote Tanzania lakini hawatambuliwi kama raia wa Tanzania, kwa sababu Tanzania, kama nchi nyingi duniani, haikubali uraia pacha. Ili kuweza kubaki katika nchi waliyozaliwa na kulia, wanahitaji visa kila baada ya miaka miwili. Kwa sasa wanatumia student visa, lakini endapo wakianza kazi, watakutana na changamoto kubwa: kupata kibali cha kazi ambacho nchini Tanzania ina gharama kubwa ya dola 1,550. Kwa hiyo, hata wakitaka kufanya kazi ndogo sana, itakuwa vigumu kwao kupata hela ya kutosha kufidia gharama hii. Uhusiano wao na Tanzania ni wa kina na wa kweli, lakini sheria za kibiurokrasi zinaharamisha vikwazo vinavyofanya kuwa vigumu kuishi katika nchi yao kwa amani. Ingawa Kiswahili ni lugha yao ya asili, na hawajawahi kuishi katika nchi nyingine yoyote, wasichana hawa wanahisi wanahojiwa kila wakati na maswali kutoka kwa Wataliano na Watanzania, kama vile: “Je, unapapenda Italy au Tanzania zaidi?” (uwa wanajibu “sijui, sijawahi kuishi Italy”), au : “Je, unajiskiaje kuishi hapa?” – kana kwamba “hapa” nchi yao ni nchi ya kigeni, kana kwamba ni vigumu kufikiria msichana mwenye asili ya Ulaya ambaye amezaliwa na kulia nchi ya Afrika, ambaye Kiswahili ni lugha ya kwanza, na ambaye anajua Tanzania, nchi yake, kama kiganja cha mkono. Watanzania mara nyingi huwa wanashangaa kusikia wasichana hawa wakizungumza Kiswahili kama wenyewe: “Je, mnawezaje kuongea Kiswahili vizuri hivi?” Kwa swali hili, huwa wanajibu, mnapaswa kushangaa kama tusingekuwa tuna jua hata neno moja la kiswahili. Maswali haya (ya kila siku ila mazito) labda ni matokeo ya dhana potofu na azma ya kuthibitisha kama, kwa kweli, mtu mwenye ngozi nyeusi hawezi kujihisi na kuwa mtu wa ulaya, na pia mtu mwenye ngozi nyeupe hawezi kuwa Mwafrika. Rangi ya ngozi haipaswi kuwa kipimo cha utaifa wako, na ingawa sifa kuu za watu fulani bado zinaonekana kwa uwazi, ni muhimu kutokufanya makundi. Maswali ya mara kwa mara kuhusu utambulisho wako siyo rahisi na mara nyingi yanaweza kuwa na athari za kihisia. Hii, kwa bahati mbaya, ni hali halisi ya watu wengi duniani na maswali haya yanayodhaniwa kuwa ya kijinga, yanasababisha hisia mbaya.

Watoto na vijana kutoka dunia nzima wanajiuliza maswali kuhusu uraia wao, ambayo haitafsiri kila mara hisia zao za kujitambua na kujihusika. Tunapojiachilia kwa dhana potofu na mitazamo ya kijamii, ambapo, muonekano wa nje unaleta moja kwa moja utaifa, tunasahau kuhusu dunia inayobadilika na kuendelea, ambapo watu hawawezi kuwekwa katika vifupisho vya mitindo ya kitaifa. Maana ya kweli ya kuishi kwenye taifa ni kuzingatia mila na desturi, na kutengeneza uhusiano wa kweli usiopingika na nchi.
Kutotambuliwa kwa uraia, ikiwa ni mfano wa maisha halisi na ya kipekee, ni pengo katika mfumo wa taasisi. Katika hali hizi, ni jukumu letu na heshima yetu kwa wengine, kuunganishwa na kujumuisha kwa umakini zaidi wale wanaoachwa nje ya mfumo kwa sababu za kibiurokrasi. Ni kwa maslahi ya wote kuishi katika jamii ambapo ushirikiano na kuheshimiana, hata katika utofauti, zipo ili kuendeleza jamii zinazovumilia na zinazoheshimu mwingine.