Mara nyingi tunajibu maswali kutoka kwa wafadhili wetu hasa kuhusu Tanzania, kazi zetu na namna ya kusimamia rasilimali kwa ajili ya kuendeleza miradi. Leo tunaka kujibu swali lingine: “Watanzania wanawasaidia?
Jibu ni “Ndio”
Kila mwezi KISEDET inapokea chakula, vifaa vya usafi wa mazingira na afya. Mara nyingine wafanyakazi wanaleta vifaa vya shule nk.
Kwa wale wanaoishi hapa wataelewa jibu hili kwa sababu kuna tabaka la kati Tanzania na hawa ndio wanatusaidia kwenye miradi yetu. Jarida letu linalenga kuwapa taarifa na kuwafundisha kuondoa dhana potofu juu ya bara la Afrika ikiwa ni hatua ya kwanza.
Kudhani kuwa kila mwafrika ni masikini ni uongo hivo hivo kwa watanzania kudhani kila mweupe ni tajili ni uongo pia. Hawawezi kufikiria kuwa kuna watu wanaoombaomba katika mji wa Rome sawa na kudhani kuwa watu wa tanzania hawawezi kutoa pesa kwa KISEDET. Sio tu watu binafsi, hata familia, marafiki kutoka makampuni binafsi na serikali wanatusaidia.
Hapa kuna mfano: kati ya 2021 na 2022 watu binafsi waliamua kuchangia euro 800 (Tsh. 1,841,849.38) ambayo ni sawa na mshahara wa daktari anayeanza kazi. Siku hizi mtu huyo ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa KISEDET.
Malengo yetu ni kuwashawishi watu wengi zaidi kote Italy na Tanzania kwa sababu zawadi inauwezo wa kuvuka mipaka. Kila mchango unaokuja Tanzania ni alama ya uelewa kulingana na uhitaji wa nchi, kielelezo cha uwajibikaji na utayari wa kufanya vizuri kuliko kusubili mtu mwingine afanye.