Lengo la kushirikiana
Lengo letu la kwanza ni kuwezesha na kutengeneza mabadiriko chanya na endelevu katika maisha ya watoto wanaoishi kipweke na kwenye mazingira hatarishi ya mitaani, kuwaokoa makundi hatarishi ili waweze kupata huduma za kiafya na huduma za VVU/UKIMWI na lishe na kuwasaidia familia masikini mitaji ya kibiashara.
Kufanya kazi na mashirika yaliyopo Dodoma yanayowasaidia watoto wa mitaani, ni kipaumbele muhimu kwa Railway Children pamoja na jiji ikijumuishwa na mikakati ya mradi wa kizazi kipya unaofadhiliwa na USAID. KISEDET ni shirika moja wapo lilijitokeza kufanya kazi na watoto wa mitaani, na kuwa sehemu ya mradi wa kizazi kipya unapokea msaada kutoka RCA katika mwendelezo wa kusaidia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Makubaliano baina ya Railway Children Africa
Dira muhimu kati ya RCA&KISEDET zinafanana na ufadhili wa RCA unatimiza maelengo ya mashirika yote mawili. Matokeo ya mafanikio ya mradi wa kizazi kipya na mafanikio ya mradi uliopita wa DFID Tanzania, RCA imefanikiwa kupata fedha za kutusaidia kukuza na kuendeleza ubora wa kazi tunazozitoa kwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ndani ya mikoa sita Tanzania imefikiwa na mradi wa kizazi kipya. Makubaliano ya shughuli hizi KISEDET pia imejumuishwa kati ya orodha ya wadau tunaoingia nao makubaliano.
Makubaliano haya yameonesha undani wa mahusiano kati ya RCA na KISEDET chini ya mradi wa kizazi kipya pamoja na wajibu wa kila mmoja wetu katika utoaji wa huduma za mradi wa ‘mawakili wa utekelezaji wa maadhimio ya umoja wa mataifa kubadilisha maisha ya watoto wa mitaani Tanzania’.
Ufadhili wa DFID ambao umeelezwa hapo juu, ni mradi wa miaka minne ambao ulianza Aprili 2018 hadi Machi 2021. Kwa kusaini makubaliano haya, KISEDET na RCA wote wanawajibika kufuata na kutekeleza matakwa na kufikia malengo mikakati iliyowekwa chini ya mradi wa kizazi kipya na kuweka mpango wa utendaji kazi ambao ulitengenezwa Februari 2019, unaokidhi vigezo vya shughuli zilizo chini ya ufadhili wa DFID. Hata hivyo malengo yaliyoorodheshwa katika makubaliano hayo yanaendana na fedha zitakazotolewa kila mwaka, makubaliano haya yatabainisha shughuli, malengo na bajeti ya mwaka wa pili wa mradi, ambao utakuwa ukirudiwa kila mwaka.