Huduma za kijamii kimataifa

Wanaojitolea? Watarajali? Waajiliwa?, hakuna jina linalofaa zaidi ya “watumishi wa jamii”

Inawezekana ulishawajua wafanyakazi wa KISEDET, watu waaminifu ambao wameshirikiana na asasi kwa miaka mingi, kufanya kazi kwa niaba ya Serikali. Wanaumoja wengine ni baadhi kati ya watoto tuliowasaidia miaka ya nyuma na sasa wako tayari kuchangia kusaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu kama walivvokuwa wao. “siamini katika misaada, ila mshikamano”, huu ni moto wa Taasisi, ambao siku zote unatuongoza: tunajisikia fahari kuwa kwenye asasi inayoendeshwa na wazawa.

Turudi hatua nyuma? hakia hapana. Kwa upande mwingine, ni fursa mpya kwa KISEDET kuboresha na kutekeleza utamaduni na ujuzi mpya ili kutoa huduma nzuri kwa walengwa wetu. Kwa hiyo, tunaweza kuwaita wanaojitolea? Jibu ni hapana. Itakuwa ni kinyume na kanuni zetu kuwapokea wageni wanaojitolea kwa kipindi cha muda mfupi. Hakika tunajari Maisha na afya za watoto na kufanya tunaloweza kuwafanya waimarike. Kwa nini huduma za kijamii kimataifa?

Kwa sababu, kama Raisi wa mkutano wa kitaifa wa idara ya huduma za kirai, Laura Milani alivosema “kuwekeza kwenye huduma za kijamii kimataifa Italy na njee, ni kuwekeza kutoa mafunzo ya uraia kwa vijana, kuleta uendelevu, ujumuishi  na mshikamano kwa jamii lengwa” tunauamini mradi huu na kwa sasa tumepokea watumishi wanne ambao wamefika Dodoma siku chache zilizopita  na wamekaa kwenye makao yetu ya kutwa na muda mfupi Shukurani. Ngoja tumuangalie mmoja baada ya mwingine ambao watakaa nasi takribani kwa mwaka mmoja.

SOFIA

Anatoka Sardinia, umri miaka 29 ni mtaaluma. Alichagua mradi wetu au mradi ulimchagua yeye. “niliposoma mradi kwa mara ya kwanza, niliwaza kuwa KISEDET na mimi tunachangamana” kilichomshawishi ni uzoefu wa miaka katika miradi inayotoa ulinzi, kufikia huduma kwa watoto na familia katika Nyanja tofautitofauti. Alituambia kuwa “ kuwajali watoto waliokatika mazingira magumu ni kuelewa changamoto katika familia hizo na kujenga mahusiano na uwezo mpya ndani ya jamii. KISEDET inafanya kazi kubwa sana na ninatarajia kujifunza mengi kutoka kwa wafanyakazi wa hapa nami nitaongezea wanapoishia. Karibu Sofia.

VERONICA

Anamiaka 28 na alizaliwa Asti, Piedmont. Alihamasika na huduma na muundo wa namna KISEDET inavowajari walengwa wake na mahitaji yao. “hakuna kilichoachwa nyuma” hali ya kusafili na lugha za kigeni, atachukulia faida ya uzoefu wa miaka mitatu katika sekta ya utalii na kuisaidia taasisi katika kuhamasisha na kufanya mradi wa utalii kuimarika. Ndoto yake ni kufanya kazi ndani ya eneo hilo kwa ushirikiano na yuko tayari kutoa uzoefu wake kwa KISEDET kuhusu harambee na kusimamia miradi. Baada ya siku chache kuwepo hapa alisema “tumepapenda kwa haraka na tunaifurahia nafasi hii”. Karibu Veronica.

CHIARA

Anatokea Paduan, umri miaka 28 ana shahada ya lugha na uhusiano wa kimataifa, amechagua kuendeleza uzoefu mrefu wa njee kutoka Austrailia hadi Vietnam, Georgia hadi Ireland ambao ulimsaidia kufanya kazi na watoto, vijana na watu wazima wenye changamoto. Alijua na kutaka kuanza safari itakayomfanya afike bara la Afrika, lakini ni mradi wetu uliomfanya kuchukua maamuzi ya mwisho: “Niligundua kuwa maono ya KISEDET yanauwiana kanuni na thamani ambazo zitanipa nafasi ya kujifunza ninapotembelea tamaduni nyingine. Nakubaliana kabisa na moto wa kuhamasisha mshikamano badala ya misaada” Karibu Chiara.

GIORGIA

Wa mwisho ni Giorgia mdogo kuliko wote kwenye kundi mwenye miaka 27 na amekua katika miji wa Treviglio mpaka alipotimiza miaka 18. Baada ya masomo ya sekondari alichagua kwenda London na Barcelona na baada ya miaka 6 ya uzoefu tofautitofauti ilimsaida kuongeza ujuzi katika Yoga na ualimu wa Kiingereza. Ujuzi huu ni sababu mojawapo ya kwa nini alichagua mradi katika KISEDET kuweka elimu na utaalam kwa walengwa wetu. Giorgia anajihisi yuko nyumbani tayari, anapenda kucheza na watoto. Karibu Giorgia.

Shirikiana nasi