Habari

Utalii

KISEDET huandaa na kuratibu safari za kitalii kwa watalii wanaotaka kutembelea sehemu maarufu kwa kuzingatia heshima ya watu na mazingira, pamoja na kutembelea miradi yetu. Kupitia safari hizi, utapata fursa ya kujionea maajabu yaliyopo Tanzania (mbuga za wanyama, bahari ya hindi na mengine mengi) na kutembelea miradi mbalimbali ya KISEDET na taasisi/asasi nyingine na utakaribishwa vizuri kwa kipindi chako chote …

Makao Ya Kutwa

Kwa muda sasa, KISEDET imeweza kuwa na makao ya kupokelea watoto wa mitaani. (Drop in Center) inayowalenga watoto wa mitaani. Lengo la mradi huu ni kuwakaribisha na kuwapa nafasi ya kuoga na kufua nguo zao, kuwa na sehemu nzuri ya kupumzikia, kupata chakula na kuwarudisha katika mazingira halisi kupitia michezo nk Kituo kinafunguliwa kila siku kuanzia 8:00 asubuhi hadi 16:00 …

Watoto Taifa la kesho

OVC ni kifupisho cha Orphan & Vulnerable Children (watoto yatima na walio katika mazingira duni) ni mradi wenye lengo la kuwasaidia watoto wanaotoka katika familia masikini, yatima na wenye ulemavu kupata elimu bora kwa maisha yao ya baadae. KISEDET inawasaidia watoto kutoka shule ya msingi, sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa kuwalipia karo , sare …

Kizazi Kipya

Lengo la kushirikiana: USAID/PACT & KISEDET. Lengo letu la kwanza ni kuwezesha na kutengeneza mabadiriko chanya na endelevu katika maisha ya watoto wanaoishi kipweke na kwenye mazingira hatarishi ya mitaani, kuwaokoa makundi hatarishi ili waweze kupata huduma za kiafya na huduma za VVU/UKIMWI na lishe na kuwasaidia familia masikini mitaji ya kibiashara. Kufanya kazi na mashirika yaliyopo Dodoma yanayowasaidia watoto …

Utalii

KISEDET huandaa na kuratibu safari za kitalii kwa watalii wanaotaka kutembelea sehemu maarufu kwa kuzingatia heshima ya watu na mazingira, pamoja na kutembelea miradi yetu.