Habari

Utumwa mpya

Wana miaka kati ya 12 na 17 na tayari watumwa wapya. Hawapelekwi Marekani lakini ni watumwa majumbani mwao, wakitumikishwa na watu wao. Wasichana, wasiosoma au kwa sababu kadhaa waliacha shule na wametoka familia masikini ambao wamepelekwa kufanya kazi kwenye familia za kitajiri katika majiji makubwa ya Tanzania. Utumwa, bila mkataba, bila mshahara, anayefanya kazi kuanzia saa kumi na moja alfajili …

Kwaheri Padri Onesimo Wissi

Padri Onesimo Wissi, alikuwa msaidizi wa Baba Askofu wa Dodoma (General Vicar) pamoja na kuwa mtu wangu wa kwanza aliyenileta Tanzania. Nilikuwa Italia nilipopokea ujumbe kuwa ameaga dunia, mpaka leo huwa siamini kuwa hili limetokea. Nilikutana nae kwa mara ya kwanza Calcinate (BG) Mach 1996 na mwezi wa saba tulisafiri kwenda Tanzania. Nilikuwa nae wakati wa utumishi wake Kigwe, kijiji …

Lugha ya Kiswahili

Lugha ya Kiswahi itadumu? Nilipofika kwa mara ya kwanza Tanzania, wanakijiji wengi na wakazi walikuwa hawawezi kuzungumza lugha ya taifa Kiswahili ila kigogo tu ambayo inazungumzwa katika mkoa wa Dodoma. Miaka 25 imepita sasa na mambo yamebadilika, watanzania wengi wanazungumza kiingereza au wanachanganya na Kiswahili. Swali ni kwanini? Inaonekana kama ni suala la kujidai. Hapa watoto wanasoma shule ya msingi …

Kuondoa dhana Potofu

Mara nyingi tunajibu maswali kutoka kwa wafadhili wetu hasa kuhusu Tanzania, kazi zetu na namna ya kusimamia rasilimali kwa ajili ya kuendeleza miradi. Leo tunaka kujibu swali lingine: “Watanzania wanawasaidia? Jibu ni “Ndio” Kila mwezi KISEDET inapokea chakula, vifaa vya usafi wa mazingira na afya. Mara nyingine wafanyakazi wanaleta vifaa vya shule nk. Kwa wale wanaoishi hapa wataelewa jibu hili …

Huduma za kijamii kimataifa

Wanaojitolea? Watarajali? Waajiliwa?, hakuna jina linalofaa zaidi ya “watumishi wa jamii” Inawezekana ulishawajua wafanyakazi wa KISEDET, watu waaminifu ambao wameshirikiana na asasi kwa miaka mingi, kufanya kazi kwa niaba ya Serikali. Wanaumoja wengine ni baadhi kati ya watoto tuliowasaidia miaka ya nyuma na sasa wako tayari kuchangia kusaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu kama walivvokuwa wao. “siamini katika misaada, ila …

Jikumbushe kuhusu Dhana potofu/Mazoea

Dhana potofu ni kitu kisichofaa, lakini kimezoeleka na watu wengi: dhana potofu ipo katika mabara yote; bara la Ulaya na Marekani dhidi ya bara la Afrika, na yapo katika bara la Afrika dhidi ya mabara mengine. Hapa chini, tutatoa mifano michache; mazoea yamejengeka katika fikra za watu tangu karne zilizopita: Kwa vyovyote tunaamini kwamba dhana potofu ni kitu cha ajabu …

Tanzania: taarifa ya Mulamula, uraia wa pacha

Chanzo: The Citizen (Dar es Salaam) Na Rosemary Mirondo Imechapwa : 6/Aug/2021 Dar es Salaam. Swala la uraia Pacha limebaki kuwa ni suala lililosahaulika kwa Tanzania, ambapo mamlaka imesimamia kuwa ni kitu kisichowezekana/ruhusiwa katika nchi. Katika mahojiano na Mwananchi Communication Limited (MCL) jana, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Liberata Mulamula alitoa mwanga kwa kusema anamatumaini …

Miaka 100 ya kuzaliwa: maadhimisho yataisha 2023

26th April 2022 imeandaliwa na Redazione Nigrizia. Tanzania inaadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Julius Nyerere. “Mwalimu Julius Nyerere (13th April 1922- 14th October 1999) anatambuliwa na watanzania wote kama baba wa taifa, ambaye waliadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake April 13. “ nawaalika watanzania wote kwa pamoja kusherekea siku hii iliyoandaliwa na waziri wa malia sili na utalii, Pindi …

Mtoto na ufadhili: kwanini tumeamua kusaidia jamii ya watoto na si mmoja mmoja

KISEDET walipendekeza kusaidia jamii kwa ujumla, na siyo mtoto mmoja mmoja. Yote hayo yalianza miaka kumi iliyopita wakati mradi wa watoto wa mitaani ulipoanza katika makao makuu ya Tanzania, Dodoma. Mchakato wa kutekeleza, mikutano, makao, na uboreshaji wa ufanisi na muda (kila mtoto anayeishi na kufanya kazi mitaani, ana historia na mpango wake binafsi) kwa hiyo, kupitia uzoefu tumejifunza kwamba …