Habari

Mwaka 2025 umeanzaje KISEDET?

KISEDET inaendelea na shughuli zake mbalimbali kupitia miradi yake tofauti. Mwaka 2025 utakuwa mwaka muhimu ambapo shughuli nyingi zitafanyika, miradi mipya itazinduliwa, na miundombinu ya makazi ya watoto kuboreshwa zaidi. Katika makazi ya Chigongwe, ujenzi wa ukarabati wa ofisi umeanza. Jengo la kwanza lililojengwa kutokana na mchango wa chama cha Maria Centro Donna cha Gorgonzola, ambalo hapo awali lilikuwa bweni …

Kuzaliwa na kujiskia “Mgeni”

Dhana ya uraia ni bila shaka mada ya mjadala inaowahusu watu wengi. Umuhimu wa kutambuliwa na taifa ni haki ya kila mmoja. Kutambuliwa na taifa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya watu, lakini ni gumu kwa wengine. Mwanadamu, kama kiumbe wa kijamii, hupata maana katika kujiskia kwamba anatambuliwa katika kundi au jamii, ambapo anajihisi kuwa na starehe kutokana na …

Picha na Ushirikiano

Namna tunavyojieleza na picha tunazoangalia, hasa katika zama hizi ambapo mitandao ya kijamii ndiyo njia ya mawasiliano, huchangia katika uelewa wetu wa dunia. Picha mara nyingi huwa ni kioo cha uhalisia, na hupokelewa kama njia halisi na yenye maana ya kuelewa maisha kwa undani zaidi. Upigaji picha, hasa kama sanaa na kama mwangaza wa ukweli wa maisha, unapaswa kuzingatiwa katika …

Uharibifu wa Kopje za Dodoma: Rasilimali Asilia Iliyoko Hatarini

Kopje ni vilima vidogo vya mawe ambavyo zinapatikana sana Dodoma, Tanzania. Mawe haya yanapendezesha sana mazingira. Muundo wake ni matokeo ya mchakato wa kijiolojia wa maelfu ya miaka. Kopje ni sehemu ya mifumo ya ikiolojia ya kipekee. Na pia, kutokana na maendeleo ya haraka ya mji wa Dodoma kama makao makuu ya nchi, tumeanza kushuhudia uharibifu wa kopje hizi kwa kasi kubwa. Hali …