Kisedet iliundwa mwaka 1998 katika kijiji cha Kigwe ili kuwapatia msaada kwa watoto kutoka familia za kimaskini na watoto yatima waliokuwa wakiishi na babu na bibi zao. Mwaka 2001, tuliamisha kituo chetu Dodoma, na kufungua kituo cha makazi ya muda mfupi na muda mrefu ‘Shukurani’ na kisha mwaka 2009, kutokana na hali ya watoto wa mitaani na vijana, Kisedet ilifungua kituo cha mapokezi cha kutwa (drop-in center). Mwaka 2010, shirika lilinunua kiwanja katika Kijiji cha Chigongwe ambacho kiko kilomita 30 kutoka Dodoma na Ikaanza kazi ya ujenzi ya makazi ya muda mrefu . Kisedet haijaendelea kwa miaka 25 kwa kupitia nyumba zake za mapokezi tu, ila kwa kupitia miradi mipya yanayolenga uboreshaji wa elimu kwa watoto na vijana, miradi ya mikopo midogo midogo na semina za elimu kwa wazazi ambazo zinalenga familia zao ili waweze kupata ujuzi kwa kujitegemea kiuchumi na kuwalea watoto wao bila kutumia ukatili wa kimwili na kisaikolojia.
Hapo chini kuna miradi yaliokamilishwa.
Pole pole Kigwe:
Kuanzia mwaka 2005 hadi 2009, Kisedet ilisimamia shule ya ufundi iitwayo ‘Chumakiu’ huko Kigwe, ambapo wasichana 30 na wavulana 47 walisoma. Ililenga watoto ambao hawakufaulu mitihani wa darasa la saba, au ambao hawakutaka kuendelea na shule ya sekondaari. Watoto hao walishasaidiwa na shirika kupitia mradi wa ‘Watoto’. Ilitoa kozi za ushonaji, uchomeleaji, useremala na kozi waliotakiwa kufanya kiulazima cha kilimo na ufugaji. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, palepale Kigwe, Kisedet ilifungua hosteli ambayo ilipokea wanafunzi wa sekondari 20 kila mwaka kutoka vijiji vya jirani ambao walikuwa wakisaidiwa na Kisedet. Wavulana hawa walisoma shule ya sekondari huko Kigwe, lakini hawakuweza kutembea na kurudi kila siku kutoka kijiji chao cha asili na walihitaji kuishi kwenye hosteli katika wakati wakisoma shuleni. Kuanzia mwaka 2007, hosteli hiyo ilipokea pia watoto wa mitaani ambao shirika walianza kufahamiana nao. Kisedet ililazimika kusitisha mradi huo kwa vile shule ya ufundi ilikuwa bure na KISEDET iliiomba serikali kugharamia mishahara ya walimu lakini serekali ikakataa na KISEDET haikuwa na uwezo tena wa kujikimu.
Darasa bora:
Kuanzia mwaka 2000 hadi 2021 mradi ulilenga shule za msingi. Kisedet iligawa msaada kwa shule hiyo, (na kwa upended moja na ushirikiano wa serikali kwenye menejimenti na kupitiamchango wa wazazi) katika ujenzi na ukarabati ya madarasa, makazi ya walimu na usambazaji wa madawati na vifaa vya kufundishia (vitabu, karatasi, chaki, kalamu, nk …). Mradi huu ulitekelezwa katika vijiji vya Kigwe, Mpinga, Chahwa, Itigi, Chigongwe na kukamilisha ujenzi ya madarasa 47, gorofa 13, ofisi 15 na usambazaji wa madawati 850 kwenye shule mbalimbali.
Chuo cha ufundi Veyula:
Mwaka 1993 kwenye kijiji cha Veyula, (kijiji ambacho kipo karibu na Dodoma), shule ya ufundi inayoitwa “umoja wa mafundi” ilianzishwa na mafundi wawili wa Veyula. Shule hiyo inakaribisha pia watoto ambao hawajamaliza masomo. Wanatoa kozi za uchomeleaji, ushonaji na useremala lakini wanataka kupanua na kujumuisha kozi za ufundi umeme na usimamizi wa hoteli. Baada ya kifo cha mmoja wa waanzilishi hao, shule ilihamishiwa eneo lingine katika kijiji hicho, na Dominic (mwanzilishi aliyebaki) ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya KISEDET kwa miaka kadhaa, alipata msaada kutoka shirika Hilo, kwa kujengwa madarasa mawili, ofisi, ukarabati wa jiko la shule, bwalo la chakula, pamoja na bweni la wanafunzi wakiume.
Afya, Vikongwe na walemavu:
Mwaka wa 2006, zahanati ilijengwa huko Mpamantwa katika wilaya ya Bahi na wakazi wa vijiji vitatu vya karibu bado wanakwenda hadi leo. Mradi huo pia ulijumuisha kusaidia wazee wa vijiji vya wilaya ya Bahi, karibu na Kigwe, kijiji paliko anzia KISEDET, kupitia chakula na matibabu. Mkoa wa Dodoma ni maarufu kwa ugonjwa wa macho uitwao ‘Trakoma’ na Kisedet ilichangia gharama kwa wazee walioenda hospitalini kwa upasuaji wa macho na kwa wazee walioathirika, ili kuwahakikishia kwamba watapona macho na hivyo uwezekano wa kutunza wajukuu zao kwa kujitegemea.Wazee wengi walikuwa wanaiishi na wajukuu wao yatima.
Kikundi cha sanaa cha Shukurani:
Kuanzia mwaka wa 2009 hadi 2017, kikundi hiki cha watoto na vijana waliokuwa katika makazi ya Shukurani walikuwa wakicheza ngoma za kitamaduni, sarakasi na nyimbo. Lilikuwa ni kundi na lengo la kuongeza uelewa kwa umma kuhusu jambo la watoto wa mitaani na vijana. Kwa miaka mingi walirekodi CD mbili na DVD na kushiriki zaidi ya mara moja katika tamasha la kimataifa la Bagamoyo. Kikundi kilisambaratika baada ya wavulana kukua na mwalimu wao kwa sababu ya shida za kibinafsi, hakuwa tena na uwezekano wa kuendelea na mradi huo.
Ni mradi unaolenga watoto, na ulianzishwa na mashirika ya kijamii ya Dodoma, yaliyowekwa chini ya uongozi wa USAID/Pact na baadaye Railway Children Africa, kukuza miradi ya VVU. Ilikuwa na lengo ya kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanaoishi peke yao mitaani wanapata huduma mbalimbali za afya ya VVU/UKIMWI na lishe bora, pamoja na kusaidia familia zenye kipato cha chini katika mazingira magumu.
Kilimo:
Mradi wa kilimo ulilenga watu wa kijiji cha Kigwe kwa kuwaonesha njia tofauti ya kutumia mbolea na kupanda mashambani ili kupata mavuno mengi zaidi.
Mradi huu ulianzishwa mwaka 1998 na ulikamilishwa mwaka 2010, tulivyofungua kituo cha Chigongwe.