Chigongwe (ilikuwa ni kijiji lakini kwa sasa imepandishwa na kuingizwa kwenye manispaa ya jiji 25 km magharibi ya Dodoma) ambapo ni makao ya muda murefu, kina lengo la kupokea watoto na vijana watakao kaa kwa muda murefu kabla ya kuunganishwa na familia zao.
Watoto na vijana wanaotoka mitaani, wanaotoka drop in center, makao ya muda mfupi ya shukurani na inapofahamika kuwa zoezi la kuunganishwa na familia zao litachukua muda murefu basi huendelea kuishi kwenye makao hayo.
Kwa miaka iliyopita, kulikuwa na uhitaji wa kupata eneo lililo njee ya mji ambalo litakuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za mafunzo, elimu nk. Sababu nyingine iliyopelekea KISEDET kutafuta eneo lingine ni kuendana na ongezeko la watoto wa mitaani Dodoma ambao wengi wao hutumia madawa ya kulevya (gundi, petrol nk)
Hivyo basi uamuzi wa kupata eneo lingine la makao Chigongwe ulifanyika ambapo uongozi wa kijiji ulitoa takribani heka 25 kwa KISEDET. Kwa kusaidia, KISEDET ilinunua mabati 140 ya kujengea jengo moja la darasa shule ya sekondari Chigongwe ambalo tayali lilikuwa kwenye ujenzi kwa thamani ya Tsh Milioni tatu (euro 1,200). Kuna mabweni mawili kwa watoto na vijana 24, na vyumba viwili self-contained kwa walezi; Shangazi Leah, Mwalimu Calvin na Mwalimu Deo. Na pia katika kiwanja hicho kuna: nyumba ndogo inayotumika kama ofisi, hosteli kwa wageni inayoitwa ‘Elena Fontana’, na karakana ndogo. Pia kuna mabwawa mawili ya kufugia samaki na banda jipya kubwa la kuku.
Bweni jipya la wanawake linaendelea kujengwa.