Mkutano mkuu wa wanachama wa Kisedet ulifanyika Alhamisi tarehe 27 Juni 2024.
Category: newsletter
Uunganisho na familia
Mara nyingi tunawahadisia kuhusu uunganishaji wa familia wenye mwisho wa furaha, lakini kwa bahati mbaya pia kuna wakati ambao familia bado ina matatizo mengi na baada ya muda, wazazi na watoto wanatengana tena katika hiyo familia.
Kwaheri Padri Onesimo Wissi
Padri Onesimo Wissi, alikuwa msaidizi wa Baba Askofu wa Dodoma (General Vicar) pamoja na kuwa mtu wangu wa kwanza aliyenileta Tanzania. Nilikuwa Italia nilipopokea ujumbe kuwa ameaga dunia, mpaka leo huwa siamini kuwa hili limetokea. Nilikutana nae kwa mara ya kwanza Calcinate (BG) Mach 1996 na mwezi wa saba tulisafiri kwenda Tanzania. Nilikuwa nae wakati wa utumishi wake Kigwe, kijiji …
Utalii
KISEDET huandaa na kuratibu safari za kitalii kwa watalii wanaotaka kutembelea sehemu maarufu kwa kuzingatia heshima ya watu na mazingira, pamoja na kutembelea miradi yetu. Kupitia safari hizi, utapata fursa ya kujionea maajabu yaliyopo Tanzania (mbuga za wanyama, bahari ya hindi na mengine mengi) na kutembelea miradi mbalimbali ya KISEDET na taasisi/asasi nyingine na utakaribishwa vizuri kwa kipindi chako chote …
Makao Ya Kutwa
Kwa muda sasa, KISEDET imeweza kuwa na makao ya kupokelea watoto wa mitaani. (Drop in Center) inayowalenga watoto wa mitaani. Lengo la mradi huu ni kuwakaribisha na kuwapa nafasi ya kuoga na kufua nguo zao, kuwa na sehemu nzuri ya kupumzikia, kupata chakula na kuwarudisha katika mazingira halisi kupitia michezo nk Kituo kinafunguliwa kila siku kuanzia 8:00 asubuhi hadi 16:00 …
Watoto Taifa la kesho
OVC ni kifupisho cha Orphan & Vulnerable Children (watoto yatima na walio katika mazingira duni) ni mradi wenye lengo la kuwasaidia watoto wanaotoka katika familia masikini, yatima na wenye ulemavu kupata elimu bora kwa maisha yao ya baadae. KISEDET inawasaidia watoto kutoka shule ya msingi, sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa kuwalipia karo , sare …