Mwaka 2025 umeanzaje KISEDET?

KISEDET inaendelea na shughuli zake mbalimbali kupitia miradi yake tofauti. Mwaka 2025 utakuwa mwaka muhimu ambapo shughuli nyingi zitafanyika, miradi mipya itazinduliwa, na miundombinu ya makazi ya watoto kuboreshwa zaidi. Katika makazi ya Chigongwe, ujenzi wa ukarabati wa ofisi umeanza. Jengo la kwanza lililojengwa kutokana na mchango wa chama cha Maria Centro Donna cha Gorgonzola, ambalo hapo awali lilikuwa bweni …

Picha na Ushirikiano

Namna tunavyojieleza na picha tunazoangalia, hasa katika zama hizi ambapo mitandao ya kijamii ndiyo njia ya mawasiliano, huchangia katika uelewa wetu wa dunia. Picha mara nyingi huwa ni kioo cha uhalisia, na hupokelewa kama njia halisi na yenye maana ya kuelewa maisha kwa undani zaidi. Upigaji picha, hasa kama sanaa na kama mwangaza wa ukweli wa maisha, unapaswa kuzingatiwa katika …

 Watumwa Wadogo

Tayari tumeshazunguumza kuhusu hili tatizo (makala: watumwa wapya 05 Januari 2023) lakini baada ya kumkaribisha A. siku mbili zilizopita, tumeona ni vyema kuizungumzia tena. A. ana miaka saba, mhudumu au tuseme mtumwa mdogo wa mwalimu wa shule ya msingi, ambaye sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi. Walivyo choka kusikia mtoto akilia na kupiga makelele kila siku wakati anapigwa na …

MRADI WA WISE: 8×1000 Kanisa la Waldesian

Mradi wa WISE unalenga kuboresha uwezo wa shirika kuendelea kutekeleza shughuli zinazoruhusu watoto wenye umri kuanzia miaka 4 mpaka 14, wanaoishi katika makazi ya muda mfupi ya Shukurani, au wale wanaoenda katika kituo cha mapokezi cha mchana (drop-in centre), kurudishwa katika makazi yao na baadae kuishi na familia zao baada ya kuunda mazingira salama kwa ajili yao.