Kizazi Kipya

Lengo la kushirikiana: USAID/PACT & KISEDET. Lengo letu la kwanza ni kuwezesha na kutengeneza mabadiriko chanya na endelevu katika maisha ya watoto wanaoishi kipweke na kwenye mazingira hatarishi ya mitaani, kuwaokoa makundi hatarishi ili waweze kupata huduma za kiafya na huduma za VVU/UKIMWI na lishe na kuwasaidia familia masikini mitaji ya kibiashara. Kufanya kazi na mashirika yaliyopo Dodoma yanayowasaidia watoto …

Utalii

KISEDET huandaa na kuratibu safari za kitalii kwa watalii wanaotaka kutembelea sehemu maarufu kwa kuzingatia heshima ya watu na mazingira, pamoja na kutembelea miradi yetu.

Mwanzoni

Mwaka 1996, mwanamke wa Kiitaliano Giovanna Moretti (Mbeleje) alisafiri kwenda Tanzania na marafiki zake wawili kwa ajili ya mapumziko. Walikaa wiki tatu katika parokia ya Kigwe kijiji kilichopo kilometa 30 kutoka Dodoma mji mkuu wa Tanzania. Kwa nini Dodoma? kwa nini Kigwe? Kwa sababu kule Italia walimfahamu padre Onesmo Wissi ambaye aliwaalika kutumia muda huo katika kijiji chake. Mwaka 1997, …

Kitabu cha picha

Ni kitabu cha picha kinachoelezea maisha ya Kisedet kila siku chenye taswira ya Romina Remigio na kupitia simulizi za Giovanna Moretti na watoto waliosaidiwa na Kisedet. Tutakizindua kitabu hiki katika tukio tunalalipanga Italia, Tanzania na ukitaka kupanga pia kufanyiwa kwenye mji wako, tafadhali wasiliana nasi.
Sasa tunahitaji msaada wako kusambaza taarifa hii, unaweza kuagiza kitabu kupitia info@kisedet.org
Fedha zitakazo patikana kutokana na kuuza kitabu hiki, zitasaidia miradi yetu Tanzania hasa kwenye kituo cha Chigongwe ambacho mpaka sasa kina watoto 19 kutoka watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani. Tafadhili sambaza na agiza nakala yako!.
Kumbuka : Kitabua hiki kimeandikwa kitaliano na kingereza na kitapatikana dunia nzima.