Mauaji ya watoto wa mitaani

Hapa tuko tena, tukisimulia mauaji ya kikatili ya watoto wawili wa mitaani. Mara ya mwisho tulikuwa tumeanza kwa kutumia sentensi ile ile: “hapa tuko tena…”Tunapaswa kuandika sentensi hii kwa muda gani? Ni lini “watu wasiojulikana” au umati uliokasirika utaacha kuua watoto wa mitaani?Toma mwenye umri wa miaka 18, aliuawa jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita. Mwarabu mwenye umri wa …

Matumaini mapya ya Meja

Ally Mussa ana umri wa miaka 24, anaishi mtaa wa Chadulu, kata ya Tambukareli, Jijini Dodoma. Kijana huyo alikaa kwenye Makao ya watoto Shukurani kuanzia mwaka 2011 hadi 2018 Alipokuwa akiishi katika Makao hayo alijiunga na shule ya msingi Chamwino kuanzia mwaka 2011 hadi 2015. Baada ya hapo alijiunga na Shule ya Ufundi pamoja na Sekondari St. Gabriel kuanzia mwaka …

Je, inawezekana kuchangia fedha katika ulimwengu wa ushirikiano bila kutumia picha za watoto?

INFO Cooperation Jumuia ya Italia kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa 17 Oktoba 2022 Kwa hakika si mara ya kwanza kwa mada hii kuongelewa na wafanyakazi katika sekta mbalimbali hasa wale wanaoshughulikia kutafuta fedha katika ulimwengu wa wafadhili. Miongoni mwa wachangishaji wa fedha hizo zipo dhana  tofauti za kifikra na kwa miaka mingi kumekuwa na mijadala kadhaa iliyopelekea tafakari kubwa …

Utumwa mpya

Wana miaka kati ya 12 na 17 na tayari watumwa wapya. Hawapelekwi Marekani lakini ni watumwa majumbani mwao, wakitumikishwa na watu wao. Wasichana, wasiosoma au kwa sababu kadhaa waliacha shule na wametoka familia masikini ambao wamepelekwa kufanya kazi kwenye familia za kitajiri katika majiji makubwa ya Tanzania. Utumwa, bila mkataba, bila mshahara, anayefanya kazi kuanzia saa kumi na moja alfajili …

Kwaheri Padri Onesimo Wissi

Padri Onesimo Wissi, alikuwa msaidizi wa Baba Askofu wa Dodoma (General Vicar) pamoja na kuwa mtu wangu wa kwanza aliyenileta Tanzania. Nilikuwa Italia nilipopokea ujumbe kuwa ameaga dunia, mpaka leo huwa siamini kuwa hili limetokea. Nilikutana nae kwa mara ya kwanza Calcinate (BG) Mach 1996 na mwezi wa saba tulisafiri kwenda Tanzania. Nilikuwa nae wakati wa utumishi wake Kigwe, kijiji …

Lugha ya Kiswahili

Lugha ya Kiswahi itadumu? Nilipofika kwa mara ya kwanza Tanzania, wanakijiji wengi na wakazi walikuwa hawawezi kuzungumza lugha ya taifa Kiswahili ila kigogo tu ambayo inazungumzwa katika mkoa wa Dodoma. Miaka 25 imepita sasa na mambo yamebadilika, watanzania wengi wanazungumza kiingereza au wanachanganya na Kiswahili. Swali ni kwanini? Inaonekana kama ni suala la kujidai. Hapa watoto wanasoma shule ya msingi …

Kuondoa dhana Potofu

Mara nyingi tunajibu maswali kutoka kwa wafadhili wetu hasa kuhusu Tanzania, kazi zetu na namna ya kusimamia rasilimali kwa ajili ya kuendeleza miradi. Leo tunaka kujibu swali lingine: “Watanzania wanawasaidia? Jibu ni “Ndio” Kila mwezi KISEDET inapokea chakula, vifaa vya usafi wa mazingira na afya. Mara nyingine wafanyakazi wanaleta vifaa vya shule nk. Kwa wale wanaoishi hapa wataelewa jibu hili …

Huduma za kijamii kimataifa

Wanaojitolea? Watarajali? Waajiliwa?, hakuna jina linalofaa zaidi ya “watumishi wa jamii” Inawezekana ulishawajua wafanyakazi wa KISEDET, watu waaminifu ambao wameshirikiana na asasi kwa miaka mingi, kufanya kazi kwa niaba ya Serikali. Wanaumoja wengine ni baadhi kati ya watoto tuliowasaidia miaka ya nyuma na sasa wako tayari kuchangia kusaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu kama walivvokuwa wao. “siamini katika misaada, ila …