Utangulizi na maelezo ya tatizo.
Watoto na watu wenye ulemavu ni moja wapo la kundi lililopo katika mazingira magumu na lililosahaulika Tanzania.hii ni kutokana na uhaba wa rasilimali zilizopo za kuwahudumia. Uwiano wa watoto wenye ulemavu katika masuala ya Elimu na Afya uko chini, ni 0.3% tu ya watoto wanaoandikishwa shuleni ni wenye ulemavu (TZ MoEVT 2013). Mbali ya uhaba wa rasilimali, pia watoto na watu wenye ulemavu wanakabiliwa na wimbi kubwa la umasikini na mazingira magumu. Wanakumbwa na utengwaji na wazazi, unyanyasaji kwenye jamii na shule. Zaidi ya hapo wanasumbuliwa changamoto za kimwili kama vile kukosa vifaa saidizi na miundombinu mibovu shuleni, walimu kutokuwa na uelewa na vifaa vya kufundishia nk.
Ukosefu wa haki za msingi kibinadamu kama vile kukosa fursa, kuondoa umasikini na ujumuishi wa watu wenye ulemavu. Mazingira yanaonesha kuwa watoto wenye ulemavu wanakuwa wamwisho kuandikishwa na wakwanza kushindwa kuendelea na masomo. Lakini pia ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi umekuwa mdogo sana kwa mikoa ya Dodoma na Singida hii ni kutokana na kutengwa hasa mambo kama hayo yanapojitokeza.
Jitihada za kupunguza tatizo
KISEDET ni mdau mmojawapo anayehusika na mshiriki mahili wa kuwajengea uwezo watoto na watu wenye ulemavu ili waweze kujitegemea. Ulemavu una eleweka kuwa ni chanzo na matokeo ya umasikini kwa familia nyingi zenye watoto wenye ulemavu. KISEDET, mbali na shughuli zake nyingine imekuwa ikasaidia masuala ya kuwainua kiuchumi watu wenye ulemavu kwa Dodoma na Itigi kwa miaka ya nyuma.
Kwa miaka mitano iliyopita, KISEDET imeweza kusaidia watoto/watu wenye ulemavu kutatua changamoto zifuatazo:
- Kutoa msaada wa kimatibabu kwa kutoa bima za afya na upasuaji kwa watoto wenye uleamvu 10 na watu wenye ulemavu 5.
- Kusaidia gharama za mazoezi ya vuingo, msaada wa viungo bandia na kupata matibabu katika vituo mbalimbali vya Tanzania (Dar es Salaam, Dodoma, Ifakara).
- Watoto na vijana wenye ulemavu, kusaidiwa kupata elimu katika shule maalumu na vyuo vya ufundi.
- Ilisaidia ujenzi wa vyoo vya watoto wenye ulemavu katika shule ya sekondari Mbabala (shule inayodahili vijana wenye ulemavu inayosaidiwa na KISEDET).
- KISEDET imejenga nyumba kwa familia ya Rahel, msichana mwenye ulemavu (nyumba yao ilianguka kutokana na mvua).
- Miongoni mwa wafanyakazi wake, KISEDET imewajiri wafanyakazi watatu wenye ulemavu (Anderson, Sesilia na Isaack).
KISEDET pia imefanya, kupitia wafanyakazi wake wa kijamii, kwa ushirikiano na wale wa serikali:
- Ziara za nyumbani na msaada wa kisaikolojia kwa familia zenye watoto wenye ulemavu, semina kwa familia na walimu, kuhusu matatizo yanayohusiana na ushirikishwaji wa watoto wenye ulemavu, na ukaguzi wa mara kwa mara nyumbani na shuleni ambao watoto na vijana hao huhudhuria.
- Kutoa msaada wa chakula cha kutosha kwa watoto wenye ulemavu na familia zao.
Kutokana na maombi ya mara kwa mara ya kuomba msaada kutoka kwa familia za watoto wenye ulemavu, KISEDET inapanga kuhakikisha msaada kwa familia hizi kwa angalau miaka mitatu kwa kuongeza huduma hizi kupitia utekelezaji wa mradi huu. Haya yote yatawezekana kupitia ufadhili wa Mradi wa Agata Smeralda huko Florence (Italia), ambao umetengwa kwa ajili yetu kutokana na ushirikiano ambao umekuwa ukiendelea tangu 2016.
KISEDET imepanga katika miaka mitatu ijayio, kutanua usaidizi wake kwa kuwalenga watoto wenye ulemavu ili kuwasaidia kufikia huduma za kielimu na kiafya. Shughuli zilizopangwa katika usaidizi huu ni kama zifuatazo:
- Kusaidia matibabu kwa kutoa bima za afya za NHIF kwa watoto wenye ulemavu 25. NHIF itasaidia katika maeneo mengi ya upimaji na matibabu kwa watoto wenye ulemavu. Gharama nyingine zitatumika kutengenezea vyeti vya kuzaliwa.
- Vifaa saidizi vitatolewa kwa watoto wenye ulemavu 10- hivi ni kama vile vifaa mwendo. Fedha iliyoombwa itasaidia KISEDET kununua baiskeli mwendo, msaada pia utajumuisha upatikanaji wa magongo na vifaa vya kujifunzia shuleni kama miwani, vifaa vya kusaidia kusikia na kuona.
- Msaada wa gharama kwa ziara maalumu kwa watoto 12, kujua kiwango na aina ya ulemavu katika vituo vinne maalumu.
- Kugharamia kukaa katika vituo vya kurekebisha tabia kwa watu wenye ulemavu wa akili kwa muda.
- Mazoezi ya viungo na usaidizi wa kisaikolojia kwa watoto 10 katika vituo maalumu.
- Msaada kwa watoto 15 wenye vifaa vya shule ikiwa ni pamoja na nyenzo za Braille, vifaa vya kusaidia masikio, miwani ya jua, shati za mikono mirefu na suruali, kofia, miwani na mafuta.
- Msaada wa watoto 4 wenye ulemavu, kupata elimu katika shule za bweni.
- Msaada wa watoto 10 wenye ulemavu kuhudhuria shule ya ufundi.
- Kusaidia watoto 5 – 10 wenye ulemavu kwenda vyuo vya ufundi.
- Kusaidia kuboresha miundombinu ya madarasa kuwa rafiki kwa kutengeneza ngazi mserereko nk.
- Kusaidia kujenga vyoo rafiki shuleni moja kwa wavulana na kimoja cha watoto wakike kwa kila shule mbili.
- Msaada katika uundaji upya wa madarasa kuwa madarasa rafiki na yanayofikika shuleni – uboreshaji wa miundo ili kuongeza njia, uingizaji hewa na darasa la kuzungumza (michoro, majina, kadi za alama/karatasi).
- Vikao na semina na familia na walimu kuhusu masuala yanayohusiana na ushirikishwaji wa watoto wenye ulemavu.
- Kufanya ziara za udhibiti mara kwa mara kwa familia na shule.
Kutoa msaada wa chakula kwa familia 10 zenye watoto wenye ulemavu na kuhimiza uanzishwaji wa vikundi vya mikopo midogo midogo na miradi midogo ya ujasiriamali.