Mrejesho wa safari

Kwa barua pepe hii tungependa kuwashukuru kwa safari yetu na pia kukupa maoni juu ya uzoefu wetu.

Kwanza kabisa, hongera kwa miradi ya KISEDET.

 Tulikaribishwa kwa ukarimu mkubwa na mara moja tulijihisi tupo nyumbani, tulikutana na wafanyakazi na Mkurugenzi Mukama ambaye alituelezea kwa kina jinsi programu za watoto zinavyofanya kazi katika makao ya kutwa na ya muda mfupi huko Shukurani, na makazi ya muda mrefu huko Chigongwe. Ukweli wote ulijaza mioyo yetu kwa furaha kwa sababu tulihisi utunzaji, umakini na upendo uliojitolea kwa miradi hii.

Tulianza safari yetu na ilikuwa yenye uzoefu mzuri.

Fulgence na Freddie walikuwa wenzi kamili wa kusafiri. Uvumilivu daima, umakini, ukarimu, uvumilivu na mwenye busara; Freddie kwa kweli ni dereva mzuri. Pamoja nao daima tulihisi raha na licha ya masaa mengi yaliyotumika kwenye gari wakati ulipita.

Sisi daima tumekaa katika maeneo mazuri, safi na daima tumekula chakula cha kipekee:
soko la Kigwe pamoja na Marimbocho, stendi wakati wa barabara ya kwenda Babati na pia njiani kurudi kutoka Arusha kuelekea Pwani ambapo siku zote tulipata mapokezi ya kipekee kutoka kwa wenyeji.
Tulishangaa hasa jioni na usiku uliotumika katika Mto Wa Mbu ambapo Freddy, kutoka Kituo cha Afya cha Diaconical, alikuwa ameandaa kila kitu kwa ajili yetu: malazi rahisi na ya ajabu karibu na hospitali na chakula cha jioni kisichosahaulika na kifungua kinywa kilichoandaliwa na wanawake wawili wema sana. Tulipenda sana ukweli kwamba tulikuwa tunasaidia jamii ndogo kwa njia hii, kama ilivyoelezewa kwetu.

Pia tulitembelea Watoto Foundation na kukaa katika Kiboko Lodge: maeneo ambayo yalituvutia vyema na ambapo tulihisi ukaribisho mzuri na shirika kamili na kwa mara nyingine tena, tulifurahi kwa sababu mchango wetu ulikuwa wa kijamii na endelevu. Tungependa kukaa muda mrefu kuchukua faida ya shughuli zilizoandaliwa na wavulana ambao kwa sasa wanafanya kazi huko.

Hatimaye, tulifika Bahari Pori huko Pangani. Hebu tuanze kwa kusema kwamba mimea ambayo nyumba ya kulala imezunguka sio kitu kidogo kuliko ajabu, pamoja na msitu mzuri wa mikoko, ni mahali pa utulivu sana na kupumzika. Francesco alikuwa mzuri na mwenye manufaa tangu mwanzo.

Tunatanguliza shukrani zetu kwa safari isiyosahaulika na pongezi kwenye miradi ya Kisedet!

 Julie & Betty.

NJIA NYINGINE ZA KUSAFIRI, NI NJIA YA SIMULIZI

Julai 2018, tulikaa Tanzania kwa wiki mbili kutembela miradi ya Kisedet kufuatia safari tuliyoshauriwa na wakala Viaggi e Miraggi. Tulikuwa familia ya watoto watatu: Iacopo miaka tisa, Marta na Giulia mwenye miaka 15. Tulikuwa na hamu kubwa ya kujifunza lakini tulikuwa na wasiwasi juu ya matatizo ya kiafya ambayo yangeweza kujitokeza. Hata hivyo ukaribisho mzuri na makazi mazuri tuliyoandaliwa na Nino, Giovanna na Julius, Baraka, Daudi waliambatana na kutuongoza kipindi chote cha safari.

Baada ya kutembelea kwa muda mfupi katika jiji Dar es saalam, tulienda Dodoma ambapo Kisedet inafanya kazi. Tulikaa siku chache Chigongwe na watoto wanaoishi katika kituo hicho. Machweo mazuri ya jua, mibuyu na hali ya hewa nzuri ya madhari ya Afrika bado vipo katika akili zetu, lakini pia furaha, ukaribisho mzuri, watoto wenye furaha, mipira iliyotengenezwa kwa vitambaa na michezo mbalimbali. Tulikuwa na siku ya kutembea kijijini na vijiji vingine vya jirani, shule, mito, vituo vya afya, kushiriki katika vipindi vya mchezo wa Giovanna wa Yoga na jioni tuliitumia kucheza mpira na kuimba nyimbo na watoto na vijana waliopo kwenye kituo.

Kwa upande wa Dodoma, tulitembelea kituo cha makao ya watoto cha Shukurani na Drop in center.

Tukiambatana na Julius (Baba kiri) na Baraka, tulienda Mwanza ziwa Victoria ambako tulikutana na watoto, vijana na wafanyakazi wa kituo cha watoto cha Cheka sana Tanzania. Asubuhi tuliitumia kushiriki michezo na shughuli mbalimbali na watoto, jioni tuliambatana na wafanya kazi wa Cheka sana katika shughuli zao mitaani za kuwatafuta watoto na kuwakaribisha katika kituo chao.

Ilikuwa mara ya kwanza kutembelea Afrika, na hatukuwa na mpango wa kufika Tanzania kwa namna yoyote ile lakini mandhari na hali ya hewa nzuri bado ipo mioyoni mwetu pamoja na watu wote wanaofanya kazi pamoja na Nino na Giovanna pamoja na maisha yao ya kiafrika yanatutamanisha/kutufanya turudi tena.

Pongezi na shukurani kwenu nyote.

Iacopo, Marta, Giulia, Silvia, Simone

Julai 2018.

Tulienda Tanzania katika kipindi cha Kiangazi na ilikuwa safari ya muda mrefu tuliyokuwa tumeipanga kutembea nchi nyinge za mbali kutoka kwetu na hatimaye tulifanikiwa.

Pamoja na wasichana wetu wenye miaka 11 na 8, tulianza safari mpya, yenye uzoefu mpya kwetu sote (hakuna hata mmoja wetu aliyewahi kufika Afrika) ambako tulikuwa tunaiona na tunaishangaa kwenye makaratasi tu.

Lakini tulipofika tu, matarajio na picha tulizokuwa nazo akilini kuhusu Afrika zilikuwa tofauti kabisa na uhalisia tulioukuta na kuuona ambao ulitufanya tubaki kushangaa tu.

Sizungumzii kuhusu fursa ya kuja au kuwa na ukaribu na Afrika na Tanzania lakini ni kuweza kuona kwa wazi kana kwamba tulikuwa watanzania, sehemu ambayo watu na kwa hali yoyote ile hatukuweza kukamilisha sisi wenyewe au kupitia wakala hatukuweza kutembelea. Shukurani za kipekee kwa KISEDET, pamoja na wafanyakazi wote waliotusaidia na kuturuhusu kuonekana kama jamii moja yenye utamuduni mmoja tofauti kabisa tulivyokuwa tukidhania.

Muhimu zaidi, tulipata nafasi ya kujionea kazi nzuri ambazo KISEDET(shirika ambalo lilianzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na Giovanna na Nino) imezifanya, na katika kushiriki katika shughuli kadhaa tulielewa ugumu na changamoto wanazozipata katika utendaji kazi wao.

Giovanna na Nino, ambao wanaendelea kufanya kazi sehemu tofautitofauti na watu mbalimbali ambao wamewafunza na kuwakuza kila siku kujaribu kuondoa mateso ya watoto wanayokumbana nayo huko mitaani na kujaribu kuwaonesha tumaini la maisha ya baadae, ambapo kwa miaka zaidi ya ishirini wengi wao wamewapa tumaini na wanamaisha bora au kuwaonesha kuwa maisha kubadilika inawezekana.

Ubinadamu uliotunzunguka na ukarimu unatufanya tuzidi kukumbuka sura, rangi, radha na maneno mazuri. Hakika tutarudi tena na pia tutajaribu kutoa msaada kidogo tutakaokuwa nao.

Lavinia &Mauro pamoja na Clelia na Frida.

Mauro ni makamu wa Raisi wa shirika la Gruppo Tanzania.

 

KURUDI TANZANIA, AU MBINU/NJIA YA UJINGA

Nilirudi Tanzania miaka 7 baada ya ziara/safari yangu ya kwanza. Kwa muda huo, niliilezea safari yangu na kuipa maneno/jina la “Moyo wa Giza” kitabu kilichoandikwa na Joseph Conrad, kilichoelezea wahusika wakuu wawili na waanzilishi wa KISEDET-Giovanna na Nino kama watu waili kama Kurtz, mhusika kwenye riwaya hiyo. Tofauti kuu ni kwamba walileta Mwanga na sio hofu katika maisha ya jangwa na ya vumbi mkoani Dodoma na mazingira yanayoizunguka.

Kwa kuongeza, nataka kuongeza kitu change kingine ninachokipenda nacho ni “HAMLET” na sio kwa sababu ni janga badala yake… ni vichekesho vyema ambavyo huwekewa rangi ya masikitiko, kama ilivyo hadidhi kwenye kitabu chetu cha “FIORI DI STRADA” ambacho kinatuonesha kwamba (nakala zipo kwa waliochelewa na wasomaji wapya wakihitaji, wasiliana nasi kukipata) Hamlet kama tunavyoona anajifanya mwendawazimu kuelewa nini kimetokea mahakamani na mtu moja alifahamu hicho, kwa hiyo alisema “hata ikiwa huu ni wazimu, kuna sababu ya wazimu wake”.

Kwa kichekesho hicho ambacho kwa sasa kuna watu wengi waliohusik, kwa kuongezea kwa wahusika… wafanyakazi wa KISEDET wameitanua KISEDET na kuwa kubwa, kwa sababu kwa muda ule ilipata wadau tofautitofauti, wakiwemo wakimataifa kwa sababu ukuaji wowote unahitaji watu, amini hicho. Ni kazi ngumu lakini pia ni ya kuridhisha na kupongezwa hasa unapofikia malengo ulijiwekea lakini hata usipofikia pia haimaanishi hujafanya chochote kwa sababu hakuna mkamilifu. Kazi mara nyingi hazitabiriki lakini kuna maendeleo yanayoonekana hasa Giovanna na Nino na wote wanaoshirikiana nao wanafanya kuwasaidia watoto na vijana kuwa mahiri na kuelewa hatua zinazochukuliwa kwa sababu hakuna mtu atakaye waamulia wao kubadilika.

Namba ya watoto na familia mbazo KISEDET imezisadia kwa miaka yote pia imeongezeka (kupata namba na idadi kamili, nashauri tembelea tovuti yetu). Ukitaka kuthibitisha hili, jaribu kuangalia picha za miaka 20 ya KISEDET kutoka (1998-2018). Kwa kuongezea kutoka kwangu (na hili pia ni mafanikio..) angalia watu na nyuso zao zenye kufurahi na kushangiria umoja kwa wakubwa kwa vijana, watoto kwa wazee.

Mafanikio mazuri ya Giovanna na Nino ni sehemu mojawapo na malengo muhimu ya KISEDET,  yanayolenga kusaidia watoto wa mitaani wa Dodoma, Chigongwe kijiji kidogo na kilichojificha kilichozungukwa na vichaka na ardhi kame ya Tanzania japokuwa karibu na kituo kuna ukijani uliotapakaa wa miti na mimea tofauti ya matunda na hata wanyama (ambao ni mbuzi waliotokana na tunzo ya vijana wetu katika michezo mbalimbali) ambapo naweza kusema ni mafanikio mengine pia.

Kati ya watoto waliokuwa mitaani kwa sasa ni wazazi japokuwa ni wadogo. Wengine ni mafundi wenye ujuzi na wafanyakazi mahiri (wahudumu, wapishi, madereva ….nk) mmojawapo ni Japhet ambaye ni dereva mzuri aliyepewa jina la Gioven kwa heshima yangu.

Kwa ufupi, nilimuacha akiwa mtoto wa miaka 14, japo alikuwa mwerevu, mahili na mwenye nguvu, nilimuona tena akiwa kijana mwenye miaka 20 mwenye nguvu zaidi. Nadhani utakubaliana name kuwa inastahili tuzo kwa kazi hii ngumu.

Na kama wasingekuwa wendawazimu tusingewahitaji tena. Natumaini kwa maelezo haya machache baadhi yenu mmetiwa moyo kuendelea kulitumia neon hili au kuliacha kabisa kama inavyosemwa kwenye Kiswahili, “Adoss che I muntu e l e gross”!!!!

Asante sana.

Giovanni Iannaccio

Makamu wa raisi Tanzania Onlus Group