Uchafuzi wa mazingira na plastiki ni mojawapo ya maafa makubwa zaidi ya mazingira kwanzia mwaka 2000: tuone jinsi bara la Afrika linavyopambana nalo.
Afrika sasa imevamiwa na plastiki, na baada ya miaka 30, matumizi yake yanakadiriwa kuongezeka mara sita kutokana na ongezeko la idadi ya watu kwa kasi cha 2% na inasababisha uongezeko wa shughuli zqa kiuchumi ambazo zina leta matumizi makubwa zaidi na matokeo yake, ni tatizo la kutupa wapi takataka.
Mpaka mwaka 2018, Afrika iliongoza kati za chini ambazo zilikuwa zinauza taka za plastiki, haswa China. Januari mwaka 2018, China ilitekeleza sera ya kupiga marufuku uuzaji wa taka za plastiki ndani ya mipaka yake,na tangu wakati huo, usafirishaji wa taka za plastiki barani Afrika ulichagua mkondo. Taka hizi zinakaribisha fursa ya kuiboresha sekta ya uchakataji tena ya plastiki ndani ya bara la Afrika badala ya kuendelea na uuzaji wa taka katika nchi za nje. Hata hivyo, sekta ya kuchakata tena plastiki barani Afrika imegawanyika sana, manaake waendeshaji mara nyingi wanaingia na kutoka sokoni, jambo ambalo linachelewesha upanuzi wa sekta hiyo.
Kutokana na ukosaji wa masoko yanayovutiwa na uchakataji wa taka , waendeshaji wengi wanaofanya kazi kaskazini la bara ya Afrika uwa wana safirisha bidhaa zao Ulayani, ambapo mahitaji ni makubwa kuliko soko la ndani. Utoaji wa nyenzo hii nchini Tanzania ni ngumu sana: kuna ukosefu wa miundombinu inayofaa na pia ujuzi wa kuchakata tena taka. Njia kuu ya kuondoa taka ni kuchoma tu, mara nyingi mitaani. Katika miji mingi ni kawaida tukuchoma taka, lakini ina madhara makubwa sana ya afya. Ukitembea mitaani, kiasi cha taka, hasa plastiki, zilizokusanyika nje za manyumba na masoko zinaonekana sana. Harufu kali ya plastiki inayochomwa kwenye mashimo ambayo ni njia pekee ya kuondoa taka ambazo haziwezi kutumika tena au kutengenezwa kuwa mbolea pia zinaonekana sana.
Sio hayo tu, matairi mara nyingi huchomwa, alafu inatoa moshi mweusi wenye sumu na ni hatari kwa afya alafu inasambaa hewani. Idadi kubwa ya watanzania wanaoishi vijijini hawana mfumo wa ukusanyaji ya taka nyumba kwa nyumba au aina nyingine ya kuondoa taka kisahihi; mara nyingi, plastiki inakusanywa na wananchi na kisha kuuzwa katika pointi chache za ukusanyaji zinazopatikana katika miji. Kwenye miji, hata hivyo, kuna mfumo wa ukusanyaji wa taka mlango kwa mlango, lakini ni
mkusanyiko bila kutofautisha taka; malori makubwa huenda kukusanya taka zote katika maeneo ambayo sio mbali sana na miji. Mahali ambapo malori makubwa hayawezi kupita, pikipiki zenye mikokoteni nyuma hupita na kukusanya taka, na kuziweka kwenye mapipa makubwa yaliyotawanyika jijini na kisha malori yanakuja kukusanya taka zilizokuwa kwenye mapipa.
Hata hivyo, mara nyingi, malori yanamatatizo, au hazipiti kwa wiki kazaa, na kwa hiyo, harufu za hizo takataka inaskika; msimu wa mvua, hata wakija kukusanya taka kwenye mapipa, takataka hulowa na kutoa harufu kali (tazama picha). Kutoka pointi za ukusanyaji wa taka, hizo taka hupelekwa katika vituo vichache vya uondoaji vya taka, vingi vikipatikana Dar es Salaam.
Mfano wa uchakataji tena nchini Tanzania ni utumiaji tena wa chupa za glasi. Baa (na baadhi za migahawa) hukusanya chupa za glasi tupu, na zinarejeshwa katika makampuni makubwa ya vinywaji, ambapo zinaoshwa na kujazwa tena kabla ya kurudishwa sokoni. Kwa bahati mbaya, bado hakuna njia ya kuchakata chupa zinazotoka nchi za nje; kwa sababu hii, (hasa chupa za divai), makampuni ya ndani huondoa lebo ya awali na kutumia tena chupa; au zinaishia katika taka zisizotofautishwa kwenye pointi za ukusanyiaji, ambapo mara nyingi zinakusanywa na watu ambao wanaziuza tena.
Nchi nyingi barani Afrika zimefanya juhudi kubwa katika miaka ya hivi karibuni ya kupunguza matumizi ya plastiki au kutafuta njia tofauti badaala ya kutumia plastiki: kwa mfano, nchi 30 kati ya 54 zimepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Tanzania sasa ni kati za nchi kwenye bari la Afrika ambazo zina nia ya kudhibiti kwa dhati matumizi ya plastiki katika himaya yao; kwa kweli, tangu tarehe 1 Juni mwaka 2019, plastiki ya matumizi ya mara moja imepigwa marufuku, lakini kwa upande moja tu kwa sababu mifuko ya plastiki, inayoitwa Rambo, imewekwa marufuku lakini wametangaza mifuko mingine ya kuuzia mchele, maharage na aina mbalimbali za kunde, karanga na kadhalika…; na mifuko haya ambayo ni membamba na madogo kuliko ya Rambo, yameanza kuchafua mazingira ya Tanzania.
Lengo ni kwamba mifuko hii, na vifaa vingine vya plastiki ambavyo hutumiwa kila siku, vizuiliwe au kubadilishwa na vifaa vingine, kwa sababu utupaji wao unadhuru sana mazingira na afya ya watu.
Takwimu na habari zimenukuliwa kutoka kwa nakala zifuatazo:
https://www.nigrizia.it/notizia/africa-sempre-piu-sommersa-dalla-plastica
https://www.plastmagazine.it/riciclo-delle-materie-plastiche-africa/