Kisa mkasa cha Peter

Hadithi ya PE ni moja wapo ya hadithi zenye mwisho wenye furaha kwa walengwa wa Kisedet na leo tumeamua kukuambia juu yake.

PE alizaliwa Moshi mwaka 1999, mji ulio kwenye mteremko wa Mlima Kilimanjaro na ni wa kabila la wachaga, mojawapo ya makabila 123 yaliyopo Tanzania.

Baada ya wazazi wake kutengana, PE na baba yake walihamia Dodoma, na bado hakuna taarifa za uhakika kuhusu mama yake alipo. Hata hivyo, uhusiano mbaya na baba yake ulimlazimisha kuondoka nyumbani na kuanza kuishi na kufanya kazi mitaani tangu akiwa na umri wa miaka minane, akiishi kwa kuomba na kukusanya plastiki na kuyauza.

Wakati alipokuwa akiishi na kufanya kazi mitaani, wafanyakazi wa Kisedet walikutana naye kupitia shughuli za uhamasishaji wa mitaani; Kwa ushauri wao alianza kuhudhuria kituo cha kutwa kila siku, na mnamo Februari 2011 alianza kuishi katika kituo cha muda mfupi Shukrani. Kwa bahati mbaya, kukaa kwake kwa mara ya kwanza kulidumu miezi michache tu, kwani mnamo Agosti mwaka huo alitoroka kurudi mitaani: haikuwa rahisi kuzoea na kufuata utaratibu na sheria za kwenye makazi. Kisedet haikukata tamaa na ilianza tena kufanya naye kazi mitaani na walifanikiwa kumfuatilia baba yake na kisha kumuunganisha na familia na kumsajili shuleni, hivyo PE alirudi kuishi na baba yake na kuendelea na shule ya msingi akiwa darasa la nne.

Kwa mara nyingine tena, baba huyo alionyesha kutokumfikiria mtoto wake, hivyo PE aliondoka nyumbani kurudi mitaani hadi siku moja, Mama Mbeleje mwaanzilishi wa shirika alimkuta amekaa chini kwenye kona ya barabara karibu na nyumbani kwake na kumuuliza alikuwa anafanya nini huko. Alijibu kwamba alitaka kurudi Shukrani na Mbeleje akamwambia “Sawa, nitakurudisha lakini jua kwamba hii ni nafasi ya mwisho”. PE, ambaye wakati huo alikuwa mtoto tu, alikuwa na nguvu ya kubadilika na tangu wakati huo na kuendelea, kila kitu kilibadilika sana kwa njia nzuri, mwaka 2015 alimaliza elimu ya msingi na kisha akajiunga na shule ya sekondari ya binafsi ambayo alimaliza mwaka 2019.

Baada ya mwaka wa nne wa shule ya sekondari, PE aliamua kutimiza ndoto yake ya kuwa muongoza watalii kwa kujiunga na “Tumaini College” Arusha Julai 2020 kwa msaada wa KISEDET, na mwaka uliofuata alipata cheti cha Utalii na Ukarimu. Baada ya hatua hiyo, PE alirudi mkoani Dodoma kusaidia katika vituo vyote viwili vya KISEDET na kufanya kazi ya kusajili laini kwa muda mfupi. Mara baada ya kuamua kuendelea na masomo yake katika fani hiyo, Oktoba 2021 PE alianza kozi ya miaka miwili katika taasisi ya Tabora polytechnic na Julai 2023 alipata Stashahada ya Utalii na Ukarimu. PE sasa anasubiri kuanza mafunzo ya utarajali ambayo atayafanya kwenye kampuni za utalii kwa kuwapeleka watalii kwenye mbuga mbalimbali za wanyama na maeneo ya kihistoria hii itamsaidia kupata uzoefu muhimu ili kutimiza ndoto yake ya kuwa mwongoza watalii.

PE alizaliwa Moshi mwaka 1999. Baada ya wazazi wake kutengana, PE na baba yake walihamia Dodoma. Hata hivyo, uhusiano mbaya na baba yake ulimlazimisha kuondoka nyumbani na kuanza kuishi na kufanya kazi mitaani tangu akiwa na umri wa miaka minane, akiishi kwa kuomba na kukusanya plastiki na kuyauza.

Wafanyakazi wa Kisedet walikutana naye kupitia shughuli za uhamasishaji wa mitaani; Kwa ushauri wao alianza kuhudhuria kituo cha kutwa kila siku, na mnamo Februari 2011 alianza kuishi katika kituo cha muda mfupi Shukrani. Kukaa kwake kwa mara ya kwanza kulidumu miezi michache tu, kwani alitoroka kurudi mitaani. Kisedet haikukata tamaa na ilianza tena kufanya naye kazi mitaani na walifanikiwa kumfuatilia baba yake na kisha kumuunganisha na familia na kumsajili shuleni, hivyo PE alirudi kuishi na baba yake na kuendelea na shule ya msingi akiwa darasa la nne.

Baba huyo alionyesha kutokumfikiria mtoto wake, hivyo PE aliondoka nyumbani kurudi mitaani hadi siku moja, Mama Mbeleje mwaanzilishi wa shirika alimkuta amekaa karibu na nyumbani kwake na kumuuliza alikuwa anafanya nini huko. Alijibu kwamba alitaka kurudi Shukrani na Mbeleje akamwambia “Sawa, nitakurudisha lakini jua kwamba hii ni nafasi ya mwisho”. PE alikuwa na nguvu ya kubadilika na tangu wakati huo na kuendelea, kila kitu kilibadilika sana kwa njia nzuri, mwaka 2015 alimaliza elimu ya msingi na kisha akajiunga na shule ya sekondari ya binafsi ambayo alimaliza mwaka 2019.

PE aliamua kutimiza ndoto yake ya kuwa muongoza watalii kwa kujiunga na “Tumaini College” Arusha Julai 2020 kwa msaada wa KISEDET, na alipata cheti cha Utalii na Ukarimu. Baada ya hatua hiyo, PE alirudi Dodoma kusaidia katika vituo vyote viwili vya KISEDET na kufanya kazi ya kusajili laini kwa muda mfupi. Mara baada ya kuamua kuendelea na masomo yake katika fani hiyo, Oktoba 2021 PE alianza kozi ya miaka miwili katika taasisi ya Tabora polytechnic na Julai 2023 alipata Stashahada ya Utalii na Ukarimu. PE sasa ameanza mafunzo ya utarajali ambayo anayafanya kwenye kampuni za utalii kwa kuwapeleka watalii kwenye mbuga mbalimbali za wanyama na maeneo ya kihistoria hii itamsaidia kupata uzoefu muhimu ili kutimiza ndoto yake ya kuwa mwongoza watalii.