Padri Onesimo Wissi, alikuwa msaidizi wa Baba Askofu wa Dodoma (General Vicar) pamoja na kuwa mtu wangu wa kwanza aliyenileta Tanzania.
Nilikuwa Italia nilipopokea ujumbe kuwa ameaga dunia, mpaka leo huwa siamini kuwa hili limetokea.
Nilikutana nae kwa mara ya kwanza Calcinate (BG) Mach 1996 na mwezi wa saba tulisafiri kwenda Tanzania. Nilikuwa nae wakati wa utumishi wake Kigwe, kijiji kilichopo umbali wa kilometa 30 kutoka dodoma. Nilikuwa na marafiki zangu wawili na padre Onesimo alituzungusha na kutuonesha maeneo mbalimbali. Tulibaki hapa kwa wiki tatu, na mwaka uliofuta tulikaa miezi mitatu, na baadae nilihamia Tanzania mpaka leo nipo.
Shukurani za kipekee kwa Padre Onesmo aliyenifanya niipende nchii hii na bara la Afrika. Kwa pamoja tulikuwa tunaenda vijijini alipokuwa akisherekea ibada za jumapili karibu na mazizi ya ng’ombe. Nikiwa nae, niliweza kuonja radha ya maisha ya kila siku katika mkoa wa Dodoma na kuunganishwa na tamaduni za kishwahili au za kigogo zilizopo Dodoma.
Nilimiliki jina la Mbeleje tokea kwake na Mzee Nkopano (aliyefariki desemba 2021). Mbeleje ni jina la kigogo analopewa mtoto wa kike aliyezaliwa kipindi cha kuandaa mashamba kwa kilimo. Limetoka kwenye kitenzi kubelega (kuandaa shamba kwa msimu wa kilimo)
Nilimpa jina la utani “Onni-absent” (kwa sababu muda mwingine alikuwa akiondoka na kurudi halafu anafanya kama hakuna kilichotokea) au “nyamone” (kwa sababu alikuwa anakula sana nyama), alikuwa na uwezo wa kuongea lugha tano na ninafikiri ndio sababu alikuwa Askofu.
Maisha yake yaliisha ghafla, akiwa na miaka 62 tu, labda kwa sababu ya shinikizo la damu au ugonjwa wa moyo. Angalau hakuteseka sana.
Kutokuwepo kwake ni sauti, sio kwangu tu ila kwa wote ambao kwa namna nyingine walikuwa wanamtegemea.
Bila yeye nisingefika hapa Tanzania na KISEDET isingekuwepo.
Pumzika kwa amani Onesimo.
Mbeleje