Tanzania: taarifa ya Mulamula, uraia wa pacha

Chanzo: The Citizen (Dar es Salaam)

Na Rosemary Mirondo

Imechapwa : 6/Aug/2021

Dar es Salaam. Swala la uraia Pacha limebaki kuwa ni suala lililosahaulika kwa Tanzania, ambapo mamlaka imesimamia kuwa ni kitu kisichowezekana/ruhusiwa katika nchi.

Katika mahojiano na Mwananchi Communication Limited (MCL) jana, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Liberata Mulamula alitoa mwanga kwa kusema anamatumaini mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 suala hili litakuwa na sura mpya.

Alisema kuwa Serikali inarasimisha njia za kisheria zitakazomtambua mtu aliyezaliwa Tanzania lakini ni raia wan chi nyingine.

Mulamula alisema kwa sasa wizara inaanda sera mkakati ya kumtambua mtu huyo, kwa malengo ya kuifanya kuwa sheria na wataliomba Bunge kuipitisha.

“zamani ilifikiriwa kuwa uraia pacha ni suala linalohusiana na katiba lakini badae ilibainika kuwa ni suala la kisheria la nchi kama vile Ethiopia na India zimelipitisha bungeni na sio kwenye katiba kwa sababu inachukua mchakato mrefu na inaweza kukumbana na vikwazo ikiwa kiongozi aliyepo madarakani atakuwa na ubia nalo” alisema.

“kushindwa kuwa na uraia pacha inatunyima fedha za kigeni na kuwanyima pia baadhi ya watu wetu haki zao za msingi” alisema Taska Mbogo (viti maalum).

Watoto wanaoishi na kufanyakazi mitaani