Picha ya Romina Remigio
Changamoto mbalimbali za kimaisha na familia hupelekea watoto na vijana kukimbilia na kuanza kuishi mitaani. Wakiwa mitaani huanza kufanya kazi mbalimbali ili kupata fedha za kuwasaidia mahitaji yao ya msingi hasa chakula na mavazi huku wakiendelea kulala mitaani. Baada ya kubani hayo, KISEDET ilianza kufanya kazi na watoto/vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani kwa kuwasaidia mahitaji ya msingi na kuwepeleka Sobber house.
Sobber house ni eneo ambalo vijana walioathirika na madawa ya kulevya (gundi,bangi,petrol nk) hupelekwa na kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo ya ushauri na saha, stadi za Maisha na shughuli mbalimbali lengo ni kuwasaidia kusahau na kuacha kabisa kutumia vilevi hivyo. Ni kazi ngumu kuwabadilisha vijana lakini KISEDET imejitahidi sana kwa kushirikiana na sobber house za Arusha na Dar es salaam (changamoto) kuwasaidia vijana wengi waliopitia huko wameacha kutumia gundi na wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii.
Mfano mzuri ni kijana Justine Tasha ambae kwa muda mrefu amekaa mitaani na alikuwa ameathirika kwa matumizi ya gundi, KISEDET ilizungumza nae na alionesha nia ya kutaka kubadilika. Shirika lilimpeleka sobber house ya Arusha mpaka sasa ameshaacha kutumia gundi na anaendelea vizuri.
Nia ya KISEDET ni kuendelea kuwasaidia watoto/vijana hao kuachana na matumizi ya gundi na madawa mengine ya kulevya kwani wengi wao hawakupenda kuwa hivyo, ni changamoto tu za kimaisha zilisababisha wajikute kwenye mazingira hayo. Tuna mpango wa kuwapeleka vijana wengi zaidi sobber house kadri tutakavoweza.
Unaweza kushirikiana na KISEDET kwa kuchangia gharama za sobber ili tuweze kuwasaidia watoto/vijana wengi zaidi. Gharama ya mtoto/kijana mmoja kwenda sobber house ni laki tatu (300,000Tsh.) na laki mbili na nusu (250,000) kwa miezi inayofuata. Unaweza tuma mchango wako kupitia akaunti zifuatazo.
BANK NAME: CRDB
A/C NO: 0150447960600
A/C NAME: KIGWE SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT
AU
CHANGIA KUPITIA M-PESA
NO. 5590401 JINA NI: KIGWE SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT. UBARIKIWE