Habari za asubuhi, Afrika!

Afrika inaendelea kuonekana kama bara ambalo limekumbwa na mvutano na vita. Lakini uhalisia ni tofauti na hivyo. Huu sio ukweli pekee. Bara ambalo asilimia 60 ya idadi ya watu wako chini ya umri wa miaka kumi na tano na wana hamu kubwa ya kuendelea kuishi. Je, Afrika ijayo itakuwaje?


Kinachoonyeshwa ni tofauti na uhalisia na kinachosemwa ni tofauti na ukweli.Hivyo Afrika inayoonekana leo, zaidi ya miaka sitini baada ya uhuru, ni bara ambalo bado limekumbwa na mivutano,vita, migogoro na hatari ya majanga ya asili na yale yanayosababishwa na wanadamu yaani madikteta katili wanaoshikiria madaraka kwa miongo mingi. Hiki ndicho kinachoonekana, je ni ukweli! Inawezekana lakini sio sehemu zote.
Afrika au Waafrika, wamedhihirisha kuwa bara lenye nguvu, ambalo linataka kuishi, kuwa na nafasi na sauti pia. Acha nitoe mfano unahusu biolojia, ambao unaweza kutumika katika mazingira ya kijamii nitakayoyaelezea.
Miaka ya 1980, wakati virusi vya UKIMWI vilipogundulika, wachambuzi wenye mamlaka, madaktari na wanasayansi walitabiri kuwa ongezeko la idadi ya watu Afrika ungebadilika, damu yao ingekuwa hasi, na makazi ya binadamu yangetoweka. Afrika bado ilithibitisha tofauti. Kwa miaka thelathini idadi imeongezeka kwa zaidi ya watu milioni mia mbili, miji badala ya kupungua imekuwa na kuongezeka na idadi kubwa ya watu wanaishi humo.


Kiukweli hii ni aina ya mfano kwa jamii. Afrika ni bara changa, asilimia 60 ya wakazi wake wako chini ya umri wa miaka kumi na tano. Ni bara ambalo lina upendo wa dhati,linaloundwa na watu ambao wanajua jinsi ya kufurahia kile wanachokipata kama fursa. Ni bara ambalo linajua jinsi ya kuishi kwa mshikamano na linakataa ubinafsi usio na maana. Hii inathibitishwa na familia, vijiji na makazi duni ambapo watoto hutibiwa na kulelewa kwa pamoja. Ni bara la ujasiri.
Ulaya yetu ya zamani (na Magharibi kwa ujumla), kwa namna nyingine ni tofauti na Afika. Umri ni tofauti,ni bara la wazee watu wa wastani, watu wenye hofu, hawawezi kuishi kwa utulivu na ambao siku zijazo ni tishio lisilojulikana, tunajikusanyia akiba benki, tunalipa bima ili kujiepusha na hatari. Kwa mwonekano huu Afrika ni endelevu na ulaya sivyo.

Shirikiana na sisi.