Mradi huu unahusisha ujenzi wa majengo mawili ya ufugaji wa kuku na uboreshaji wa mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia maji kidogo (mfumo wa matone) katika makao ya watoto ya Chigongwe Family.
Tuna furaha kubwa kuwajulisha kuwa ujenzi wa banda la kuku unakaribia kukamilika na hivi karibuni litaweza kutumika kwa kufuga kuku wa nyama na mayai.
Muundo wa banda la kuku ulijengwa kwa matofali ya saruji, mabati ya chuma na paa ya mbao, tumehakikisha kwamba kuna mzunguko wa hewa na tumeweka taa , na kuna maeneo ambazo wanaweza kukaa njee.
Kibanda hicho kina ukubwa kulingana na idadi ya wanyama wanaopaswa kufugwa (wanyama 500, ambao 400 ni kuku wa nyama, na 100 wanaotaga). Eneo la nje litawawezesha kuku kuishi kwa kawaida na tutawapatia vitamini, antioxidants na vitu vingine muhimu kwa ukuaji wa afya wa ndege na tufuge nyama yenye ubora.
Hatimae tumemaliza kujenga kibanda cha kuku na sasa kazi ya kuboresha mfumo wa maji kimeanza!
Mradi huo ni pamoja na:
- ujenzi wa tanki ya saruji ya lita 20,000
- ununuzi wa pampu ya umeme (yenye nguvu 5 HP) kwa kusukuma maji
- ununuzi wa mita 2000 za mabomba kwa mfumo wa kumwagilia kwa matone na vifaa vingine vya umwagiliaji (ni bora zaidi kuliko umwagiliaji kwa mkono)
- tutaongeza matenki mwaili ili kufikia uwezo wa jumla wa lita 20,000.
Ardhi ya makao ya Chigongwe Family ina eneo la takriban ekari 40 ambapo takriban 40% ni kwa matumizi ya kilimo na kwa sasa umwagiliaji unafanywa kwa mikono, kazi inayohitajika muda mrefu na nguvu pamoja na matumizi makubwa ya maji.
Miradi hii kwa hiyo italeta faida kubwa katika suala la uhuru wa kiuchumi wa kituo cha Kisedet huko Chigongwe, usambazaji wa chakula safi na bora kwa vijiji vya jirani, na itawapa watoto fursa ya mafunzo na kazi katika sekta ya kilimo.
Tutaendelea kueleza kuhusu maendeleo ya kazi!