Help street children in Tanzania

Home>Habari>Uncategorized>Siku Za Nyuma

Asubuhi hii baada ya mvua kunyesha usiku, nilipoangalia njee kupitia dirishani niliona frangipani(aina ya maua) chini na ilinisikitisha sana. Naamini hata miti pia ina moyo. Nilichukua simu yangu na kujaribu kumtumia ujumbe Mama Steve, sikuwa nimezungumza nae kwa muda mrefu kidogo lakini niliacha tu kiende. Baada ya mtu wa bustani kumalizia kumwagilia miti na kuniruhusu nipite (alianguka mbele ya geti) simu ikaanza kuita, Mama Steve! Sawa! Najua kwamba mm ni telepathiki na huu ni uthibitisho wa maranyingi (na hapa nafikiri juu ya Pierina wangu akiwa anasoma kipeperushi)

Nilipokea na mama Steve aliniambia kuwa nyumba yake yenye vyumba viwili ilianguka kutokana na mvua, nilimjibu kuwa ninaenda ofisini nikifika tutaenda na wenzangu kumuona. Tulifika eneo la tukio na nyumba ya tope ilikuwa na ufa mkubwa, binti mkubwa alituambia “ hapa jua likiwaka tu nyumba hii itaanguka yote” na mwenzangu Daudi alithibitisha mbinu hii. Mandago ambaye ni mratibu wa KISEDET alimhakikishia mama Steve kuwa tutamtafutia fedha za kupanga vyumba vingine ambavyo atavitumia kukaa na atatakiwa kurudisha taratibu kodi hiyo kwenye shirika japo nyingine tutakuwa tumemsaidia.

Tuliondoka na kwenda upande mwingine wa mji kwa Bibi Luka, mwanamke mwenye ulemavu ambaye anaishi na watoto wawili yatima (wajukuu), yeye tulikuwa tumemsaidia kumpatia baiskeli ya miguu mitatu yenye mota. Pia tulimpelekea chukula. Bibi Luka anaendesha maisha yake kwa kuuza mkaa, alizidi kutupa Baraka kwa kusema “mbarikiwe sana” na baadae aliniambia:” Mbeleje unajua nyumba yangu haivuji tena hata mvua ikinyesha? Namshukuru Mungu mwaka huu umekuwa mzuri kwanza mmekarabati nyumba yangu iliyokuwa ikivuja, sasa baiskeli, namuomba Mungu kila siku awabariki, hicho tu ndo naweza kuwarudishia.

Nimeishi Afrika kwa miaka 23 sasa,  lakini matumaini haya, nguvu na mafanikio yamekuwa yakinitia moyo! Jana nilichanganywa na urasimu usioisha, lakini ninapoonana na watu kama hawa nasahau yote moyoni mwangu, nafikili kuendelea kufanya ninachokifanya kila siku kwa sababu sitaweza kufanya hivyo mahala pengine popote.