Makao ya Shukurani hupokea watoto na vijana wanakuja kutoka mitaani na ambao hukaa kwa muda mfupi kabla ya kuunganishwa na familia zao au kwa wale ambao wameathirika sana na aina mbalimbali za ukatili na wanahitaji sehemu nzuri ya kukaa.
Wanaweza kukaa kwenye makao hayo kwa muda usiozidi miezi mitatu na tukiona kazi ya kumuunganisha na familia inachukua muda murefu, au ikiwa muda huo haiwezekani basi mtoto huhamishiwa Chigongwe kwenye makao ya muda mrefu, ambapo wanaweza kukaa kwa muda murefu. Wanapokuwepo huendelea kupata huduma nyingine muhimu kama vile elimu, matibabu, milo mitatu na upendo.
Maafisa ustawi wa KISEDET huendelea na shughuli tofautitofauti za kuwaweka sawa kisaikolojia na kuhakikisha kuwa wanarudi katika familia na jamii zao. Baadhi ya shughuli hizo ni Yoga na tafakari, uchoraji, vipindi vya mtu mmoja au kikundi vya ushauri, elimu ya afya, sarakasi na nyimbo za sili (ngoma) nk
KISEDET siku zote hufanya kazi kwa kushirikiana na serikali katika kufuata maelekezo kulingana na miongozo ya Tanzania ya ufanyaji kazi.