Maono ya KISEDET:
Kuiwezesha jamii kiuchumi na kuwa na maisha yenye utu.
Utume/dira:
kuinua hali za kijamii na kiuchumi kwa jamii zinazoishi katika mazingira magumu/hatarishi kwa kuwawezesha kutambua fursa zinazowazunguka.
Lengo kuu:
kuwa na jamii ambayo makundi hatarishi/ yanayoishi katika mazingira magumu yanafurahia haki zao za msingi na kuwa na maisha yenye utu.
Maadili ya Shirika
- Maendeleo shirikishi: Tunaamini kuwa wadau wote wanahitajika kujihusisha na mambo ya maendeleo.
- Haki sawa na huduma bora kwa watu wote bila upendeleo wowote. Tumejidhatiti kutoa huduma kwa watu wote pasipo kuzingatia mambo ya siasa, dini, jinsia, umri, ukabila, rangi au elimu.
- Usawa wa kijinsia: wanaume na wanawake wote lazima wajihusishe kwenye maendeleo kwa usawa.
- Uwazi na uwajibikaji: Tunatoa nafasi ya kidemokrasia inayotoa uwazi na kutoa mfumo mzuri wa kuongoza. Pia tunawajibika kwa wadau wote.
- Uendelevu: Tunaamini jamii ina watu ambao wanaweza kutambua fursa na kuzitumia kwa maendeleo yao.
- Mitandao na ushirikiano: tunaamini katika kudumisha na kujenga mahusiano na ushirikiano mzuri na wadau mbalimbali ili kutoa huduma bora.
- Hamasa na kujituma kwa nguvukazi: nguvukazi ya KISEDET ni kitu muhimu sana na kila mtu ni sehemu ya furaha katika familia ya Shirika. KISEDET itajitahidi kudumisha hamasa ya nguvukazi na kujituma kwa kufanya kazi katika usimamizi mdogo.
TIMU YETU.
Kitu muhimu sana katika shurika. Zaidi ya watu 30 wanafanya kazi ndani ya KISEDET katika kutimiza shughuli za shirika Tanzania.
Kila siku, kwa kujidhatiti na kwa moyo wa upendo, tunamshukuru Enidy, Issa, Deusdedith, Hamisi, David, Leah, George, Sechelela, Mama Peter, Peter, Edwin, Laurent, Ibrahim, Yohana, Maimuna, Mama Mika, Anderson, Isack, Leonard, Mandago, Sabina, Johny, Fulgence, Alvin, Aidan, Steven, Freddie, Saidi, Ismail, Giovanna Mbeleje.