Machi 2, 2021 Dodoma (Na Giovanna Moretti Mbeleje)

street child

Leo katika kituo cha malezi ya kutwa cha KISEDET, F…. mtoto ambaye tumejaribu kwa miaka kadhaa kumtoa mitaani, baada ya afisa wa shirika kuchukua chupa ya gundi ambaye alikuwa anaivuta, ameshindwa kujizuia na kuchukua kisu na kuanza kututisha (kwa sasa asilimia kubwa ya wafanyakazi wetu wanafanyia kazi nyumbani). Ameanza kurusha mawe, kwa bahati nzuri hajampiga mtu yeyote/kitu chochote,  mfanyakazi wetu mrefu na mwenye nguvu Fulgence hakuwepo, tunashukuru Mungu Konjani afisa msaidizi kutoka idara ya familia alikuwepo na akaweza kumdhibiti na kumtoa njee ya kituo kwa msaada wa Edwin.

Baada ya saa moja, nilipokuwa nafanya kazi na Tanakilishi (computer), kuna mtu aligonga mlango kumbe alikuwa ni yeye F. sikuogopa kwa sababu namfahamu huyu kijana kwa zaidi ya miaka nane na nilijua fika hakumuumiza mtu yeyote. Niliposoma kitabu kinachohusiana na watoto wa mitaani, hata kama wakifanyiwa vurugu wanakuwaga tayari kujirudi na hivi ndivyo walivyo kwa sababu wanajua watu waliowatelekeza katika nyakati ngumu.

Alikaa mbela yangu na kuomba msamaha, lakini alikuja Konjani (bila F kujua)  na kuniuliza “kila kitu kiko sawa?” nikamjibu ndiyo, nakawa na muda kidogo na F na baadae tukamwita Konjani tena na kwa pamoja tukamwambia kuwa hii itakauwa ni nafasi ya mwisho tutakayompatia. F alikaa kwenye makao yetu ya muda mfupi na mrefu na alitoroka. Tulimchukua kumpeleka Arusha na matokeo yalikuwa ni yaleyale. Kama anataka KISEDET iendelee kumsaidia, masharti ni kwamba, kwanza itabidi akubali kwenda kwenye kituo cha kuwalea na kuwatunza waoto wanaotumia madawa ya kulevya ili kuwabadilisha ambapo kwa mwezi mmoja inagharimu kiasi cha euro 80 (Tsh 200,000) na inabidi akae angalau kwa miezi mitatu, vinginevyo hatutakuwa na kitu kingine cha kumsaidia. Tulimwambia arudi siku ya ijumaa na majibu. Na hii ndio sababu nimemnukuu Che mwanzoni kwa sababu kazi zetu ni kuwahudumia watoto ni hii ndio sababu tunatakiwa “kuwa imara bila kupoteza uvumilivu na umakinni katika kuwahudumia”