Chigongwe (ilikuwa ni kijiji lakini kwa sasa imepandishwa na kuingizwa kwenye manispaa ya jiji 30km magharibi ya Dodoma) ambapo ni makao ya muda murefu, kina lengo la kupokea watoto na vijana watakao kaa kwa muda murefu kabla ya kuunganishwa na familia zao.
Watoto na vijana wanaotoka mitaani, wanaotoka drop in center, makao ya muda mfupi ya shukurani na inapofahamika kuwa zoezi la kuunganishwa na familia zao litachukua muda murefu basi huendelea kuishi kwenye makao hayo.
Kwa miaka iliyopita, kulikuwa na uhitaji wa kupata eneo lililo njee ya mji ambalo litakuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za mafunzo, elimu nk. Sababu nyingine iliyopelekea KISEDET kutafuta eneo lingine ni kuendana na ongezeko la watoto wa mitaani Dodoma ambao wengi wao hutumia madawa ya kulevya (gundi, petrol nk) Hivyo basi uamuzi wa kupata eneo lingine la makao Chigongwe ulifanyika ambapo uongozi wa kijiji ulitoa takribani heka 25 kwa KISEDET. Kwa kusaidia, KISEDET ilinunua mabati 140 ya kujengea jengo moja la darasa shule ya sekondari Chigongwe ambalo tayali lilikuwa kwenye ujenzi kwa thamani ya Tsh Milioni tatu (euro 1,200). Mpaka sasa kuna nyumba mbili ndogo zinazochukua takribani watoto 24 na vyumba vya kulala maafisa wanaowahudumia watoto ambao ni Shangazi Leah, mwalimu Issa na Issac. Watoto/vijana wanaokaa hapo husoma katika shule ya serikali ya msingi na sekondari iliyopo karibu na eneo hilo.