Help street children in Tanzania

Home>Habari>Uncategorized>Huduma Za Jamii Kimataifa 2021

Gruppo Tanzania Onlus & Kisedet NGO zinatoa nafasi!!

Mwaka huu tumeamua kuchukua nafasi katika matangazo ya serikali kwenye idara ya vijana, sera na huduma za kijamii kimataifa, kuwasilisha shughuli za miradi yetu. Tunafikiri huduma hizi ni muhimu kuzitambulisha kwa vijana ili wajue shughuli tunazozifanya  na kupanua mawasiliano. Wanaojitolea katika huduma za kijami huleta nguvu, ujuzi na maarifa pamoja na mawazo mbadala. Kuwa na watu wanaojitolea katika shughuli zetu za kijamii husaidia kubadilishana watu na utaalam katika Nyanja mbalimbali kwetu na kwao.

Kusambaza ujuzi/taarifa za taasisi yetu Italia na Tanzania ni njia muhimu ya kusambaza utamaduni wenye umoja na ujuzi kati ya watu, kuchangia elimu ya uraia katika ufahamu mpya.

Vijana lazima wajue ushirikiano na  kujitolea sio dhana iliyoandikwa kama rasilimali tu: inamaanisha kufanya kazi ili kuwasaidia watu wenye uhitaji kurudisha utu wao na kuwawezesha.

Kuwapa nafasi vijana wa Ki-Italiano kupata uzoefu ni njia mojawapo tunayoitumia ili kutengeneza uelewa mpana wa kijamii dhidi ya amani na utamaduni wa kushirikiana.

Huduma za jamii kimataifa ni nafasi muhimu kukuza na kuwawezesha watu binafsi na utaalamu wao.

Tangazo hili liko wazi na linawahusu vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 29, raia wa Italy au wanaoishi Italy. Wanachotakiwa kufanya ni kujichagua wenyewe kwa tangazo litakalo fuata, ambapo tutaleta mradi wetu wa “ Tuwajali watoto”.

Kaeni tayari, taarifa zitatolewa hivi karibuni.