Uuzaji chakula. Mwanzo mzuri
Melina (21), Mage (22) na Kashinde, picha katikati, walijiunga na kikundi cha VITUNU tangu January 2019 wakitamani kushirikiana katika maisha kama wasichana wengine. Kikundi hicho kinapatikana Chang’ombe karibu na makazi yao. Kikundi hicho kina wasichana watatu ambao wameamua kushirikiana kupitia uzoefu wao na kusaidiana kama wanakikundi. Kwa Melina, Kashinde na Magreth maisha yao hayakuwa rahisi kwani walijikuta wakipata ujauzito kabla hata ya kufikisha miaka 18, bila hata kupata msaada na kulaumiwa na wenzi wao kutokana na mimba zisizotarajiwa. Hali ilikuwa mbaya sana kwa mage ambapo mchumba wake alimtoroka na kumuacha na hali ya sintofahamu na mazingira magumu, hivyo aliishi kwa dada yake ambaye ana vyumba viwili vilivyojengwa kwa matofali na kuezekwa na udongo.
Kwa kushirikiana na wanagenzi wa Chang’ombe, walimsaidia afisa vijana kitoka KISEDET kukutana na Mage na marafiki zake wawili ambao walikuwa tayari kushirikiana kwenye umoja huo. Wakati wa mafunzo/semina za biashara kati ya washiriki49 walioshiriki mafunzo hayo, nao walikuwa wamojawapo wa vijana waliochagua kusoma fani ya upishi.
Kutoka shule hado biashara.
Wasichana hawa watatu walishiriki mafunzo ya mbinu za kuunda vikundi kama vile semina ya siku moja, ujuzi wa kimaisha na kuwaunganisha kwenye vyuo vya ufundi kushirika fani ya upishi kwa muda wa miezi mitatu. Baada ya kukamilisha mafunzo hayo katika chuo cha Boboya waliamua kujiajiri kwa kumiliki mgahawa wa chakula katika eneo la Chang’ombe Dodoma. Baada ya kupewa mitaji ya kuanzia, wasichana hawa watatu hawakuamua kuachana baada ya kumaliza mafunzo hayo bali waliamua kukubalina na kufanya kazi pamoja ya biashara.
KISEDET inajuvunia Mage, Kahinde na Melina sio kwa sababu walihitimu vizuri mafunzo yao bali nia na dhamira yao juu ya biashara ya uuzaji chakula. “matarajio yangu ni kuona tunakuwa na kumiliki mgahawa mkubwa utakao hudumia wateja wengi kwa mara moja”alisema Melina. Mbali ya changamoto wanazokumbana nazo bado wasichana hawa wanajitahidi kukabiliana nazo, ambazo ni ushindani mkubwa wa wafanya biashara walio karibu nao na mtaji wao kuwa mdogo amba ni Tsh, 25,000. Mojawapo ya mbinu wanazotumia ni kufanya biashara kupitia simu ambapo watu hipiga simu na kuweka oda na wanapopika huwasambazia majumbani. “tunawahudumia wateja wetu kulingana na uhitaji wao, hatuwezi kuwa na kila aina ya chakula wanachohitaji kwenye mgahawa wetu lakini tunajitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma wanayoihitaji hasa chakula kitamu” Mage alisisitiza. Kwa sasa mtaji wao umekuwa hadi Tsh. 45,000/=
“Malengo yetu ni kutoa huduma bora za chakula kwenye mgahawa bora. Maisha yetu yamefanikiwa kutokana na taarifa na mafundisho mazuri ya KISEDET wanayotupatia na kwa kweli tunawashukuru sana kwa hayo yote. Na kama mtahitaji huduma katika shughuli zenu au kututumia kama mfano msisite kufanya hivyo”alisema Kashinde.
“nyinyi ni mfano mzuri wa kuigwa katika jamii kama mtajikita na kutumia vizuri zana na maarifa mliyopewa mnaweza kuwa wapishi wazuri na kupatiwa tenda kubwa na mtafanikiwa” Theresia Ntuli afisa maendeleo kata ya Chang’ombe alipo watembelea wasichana hao.